Mungu Mwana – Mwongozo wa Mkufunzi: Capstone Module 10 Swahili Mentor Guide
/ 7 9
M U N G U M W A N A
Ni Imani Iliyopotoka au Ni Tendo la Kujihusisha tu na Wenye Dhambi?
“Harakati za watu wa ndani” ni vuguvugumuhimu na lenye nguvu ya RohoMtakatifu katika umisheni leo. Nchi nyingi sasa hazifikiwi na watenda kazi wa Kikristo wa kigeni, wamishonari, au “watengeneza mahema”—Wakristo wanaoenda katika “mataifa yaliyofungwa” kufanya kazi katika nafasi na sekta za kidunia kwa lengo la siri la kueneza Injili. Wabuddha na Waislamu wengi (miongoni mwa wengine) wanakuja kwa Kristo, lakini, wakidumisha desturi na mahusiano yao ya awali ya kiutamaduni kwa ajili ya “kujihusisha na watu wa nchi zao kwa lengo la kueneza Injili.” Kwa mfano, baadhi ya “wafuasi wa Kristo” Wabuddha wanakiri kuwa wanamwamini Yesu, lakini wanakataa kutumia neno “Mkristo,” ambalo katika miktadha mingi ya kitamaduni ni sawa na kusema “Mimi ni mfuasi wa tamaduni za Magharibi na nimeukana utii na uaminifu wangu kwa utamaduni wangu na watu wangu.” Kuna ripoti za vuguvugu kubwa ndani ya jumuiya za Kiislamu za watu binafsi ambao wamekuja kwa Yesu kwa imani lakini bado wanasalia ndani ya mipaka ya kitamaduni ya Uislamu na jamii za Kiislamu. Wakilinganisha mazingira yao na hali ilivyokuwa kati ya dini ya Kiyahudi na Ukristo wa karne ya kwanza, waumini hawa wanaamini kwamba hakuna njia nyingine ya kuwafikia mamilioni haya bila kujitambulisha kama mmoja wao, jambo ambalo lina maana ya kudumisha mahusiano nao ndani ya mitandao yao ya kidini na kitamaduni. Je, hii ni imani iliyopotoka au, kama alivyofanya Yesu, ni kujihusisha na wenye dhambi kwa ajili ya wokovu wao? Katika makanisa yetu mengi leo, mafundisho kuhusu Yesu wa Nazareti “yameenda uhamishoni”. Maadili, kanuni, na amri za Bwana Yesu mara nyingi hazizingatiwi na badala yake zinazopewa kipaumbele ni «kanuni na sheria» za baraka na ustawi wa maisha, huku maneno magumu ya Yesu yanawekwa kapuni ili watu wasikilize kauli za dhahabu za wainjilisti wa kwenye runinga ambao huwahubiria watu imani za utajiri, afya, furaha, na mafanikio. Kwa kweli, katika hali mbaya sana, wale wanaougua magonjwa na umaskini wanalaumiwa tu kwamba wanateseka kwa sababu wameshindwa kutumia kanuni za Maandiko, ambazo mara nyingi ukizichunguza unagundua hazimo katika mafundisho ya Kristo. Fundisho hili la mafanikio ni maarufu sana leo kiasi kwamba wengi hufikiri kwamba ndilo kiini cha fundisho la Yesu mwenyewe kuhusu Ufalme. Fikra chanya, ustawi na baraka, afya na faraja – hii imekuwa kauli mbiu inayochukua nafasi ya fundisho la Kristo la unyenyekevu na kuchukua msalaba wetu na kumfuata. Ni kwa njia zipi tunapaswa kufundisha ubinadamu wa Kristo leo; Ni kweli kwamba maisha yake yanatupa kielelezo cha kufuata au tuamini kwamba Kristo aliteseka katika mwili ili tuwe na utele usiojumuisha aina ya mateso na uhitaji alioupitia ? Yesu wa Nazareti au Kristo wa Imani
3
2
4
Made with FlippingBook - Share PDF online