Mungu Roho Mtakatifu, Kitabu cha Mwanafunzi, Capstone Module 14 Swahili Student Workbook

1 0 4 /

M U N G U R O H O M T A K A T I F U

(2) Matendo 1:4-5 – Hata alipokuwa amekutana nao aliwaagiza wasitoke Yerusalemu, bali waingoje ahadi ya Baba, ambayo mlisikia habari zake kwangu; 5 ya kwamba Yohana alibatiza kwa maji, bali ninyi mtabatizwa katika Roho Mtakatifu baada ya siku hizi chache 3. Makanisa yanayofundisha kwamba kuna tukio tofauti la ubatizo wa Roho Mtakatifu linalofuatia lile linalotokea wakati wa kuongoka ni pamoja na: Kanisa Katoliki la Rumi*, kanisa la Holiness , na makanisa ya Kipentekoste. Katika sehemu inayofuata, tutakuwa tukichunguza misimamo ya makanisa ya Holiness na ya Kipentekoste. a. Ubatizo katika Roho Mtakatifu: Mtazamo ya makanisa ya Holiness (1) Mifano ya makanisa ya Holiness ni pamoja na: Kanisa la Mungu (Anderson, IN), Kanisa la Mnazareti, Kanisa la Kimethodisti Huru, n.k. (2) Msingi wa kimaandiko : fikiria kwa upana kuhusu ushuhuda wote wa Maandiko badala ya kuanza na vifungu vichache muhimu kuhusu mada fulani na kujaribu kuvitumia peke yake kujenga hoja. (3) “Utakaso kamili” (wakati mwingine huitwa ukamilifu wa Kikristo) unawezekana katika maisha haya na Mungu anatazamia tuutafute kwa bidii lakini haupatikani kwa juhudi za kibinadamu tu (ni kipawa cha neema), na kwa sababu hiyo, *Kwa ufupi, mtazamo wa Kanisa Katoliki la Rumi kuhusu ubatizo wa Roho ni kama ifuatavyo: Roho Mtakatifu hupokelewa katika ubatizo wa maji ili kumuunganisha mwamini na Kanisa. Huu unatazamwa kama “ubatizo wa Roho Mtakatifu” ulioahidiwa na Yesu ( Katekisimu ya Kanisa Katoliki , uk. 190, 312, 321-22). Hakuna utofauti muhimu kati ya “ubatizo wa maji” na “ubatizo wa Roho.” Hata hivyo, katika theolojia ya Kanisa Katoliki la Rumi “sakramenti ya Kipaimara ni muhimu kwa ajili ya ukamilisho wa neema ya ubatizo. Kwa sababu kupitia sakramenti ya Kipaimara, [wanaobatizwa] wanafungamana kikamilifu zaidi na Kanisa na wanajazwa nguvu maalum za Roho Mtakatifu” ( KKK , uk. 325-26). Tendo hili linaeleweka kama kuongeza karama za Roho Mtakatifu kwa mwamini ( KKK uk. 330). “Ujazo” huu wa Roho ( KKK uk. 326) unapokelewa kwa kuwekewa mikono, kupakwa mafuta, na maombi ya Askofu ( KKK uk. 329). Kwa hiyo, kama vile ilivyo katika theolojia ya makanisa ya Holiness na ya Kipentekoste kuna tukio la hatua ya pili ambapo mtu anapokea utimilifu wa Roho Mtakatifu.

Ni muhimu sana kukumbuka kwamba waamini wa makanisa ya Wesley hawaufikii ufahamu wao wa kibiblia wa utakaso kwa mfumo wa tafsiri za kimantiki unaotokana na uthibitisho kwa njia ya Maandiko au hoja. Imani yao juu ya uwezekano wa kufikia ukamilifu katika upendo katika maisha haya na ule utakaso wa moyo kwa imani unaofuata baada ya kuhesabiwa haki hutokana na jitihada zao za kuyatazama Maandiko katika ujumla na ukamilifu wake. ~ Melvin Dieter, former provost of Asbury Theological Seminary. Five Views on Sanctification . Grand Rapids: Zondervan HarperCollins. 1987.

3

Made with FlippingBook Digital Proposal Maker