Mungu Roho Mtakatifu, Kitabu cha Mwanafunzi, Capstone Module 14 Swahili Student Workbook

1 0 8 /

M U N G U R O H O M T A K A T I F U

(b) P ili, “utakaso kamili” ambapo Roho humweka huru mwamini kutoka katika dhambi ya makusudi na kumkamilisha mwamini katika upendo (jambo ambalo makanisa ya Holiness yanaita ubatizo katika Roho Mtakatifu). (c)  Tatu, ubatizo katika Roho Mtakatifu, unaothibitishwa na kunena kwa lugha, ambapo Roho humjalia mwamini uwezo kwa ajili ya utume na huduma (ufafanuzi sawa na mtazamo wa Kipentekoste). » Wakristo wanakubaliana kwamba ni lazima, kwa namna fulani, Roho aje juu ya mtu wakati wa kuokoka kwake ili apate kusafishwa kutokana na dhambi na kuunganishwa na Kristo. » Baadhi ya Wakristo (mtazamo wa makanisa ya Reformed ) wanaamini kwamba maisha yote ya Kikristo yanahusu kujifunza zaidi na zaidi kuhusu uwepo wenye nguvu wa Roho Mtakatifu ambao mtu huupokea pale tu anapookoka. » Wakristo wengine (wa Holiness na wa Kipentekoste) wanaamini kwamba Kitabu cha Matendo ya Mitume kinafundisha kwamba kunapaswa kuwa na matukio zaidi ya Roho Mtakatifu katika maisha ya mwamini, ambapo mkristo atapokea nguvu kubwa zaidi kwa ajili ya maisha matakatifu na ufanisi katika huduma. » Wakristo wote wanapaswa kukubaliana kwamba kujifunza kutegemea nguvu za Roho Mtakatifu ni jambo lenye umuhimu wa kwanza ili kuwa mtu wa Mungu na kufanya kazi yake. » Mwanatheolojia J. I. Packer analeta ufafanuzi tofauti wa ubatizo wa Roho katika makubaliano ya pamoja anaposema, “Kwa kuwa maisha yenye ubora wa kitume ni adimu na wa kutamanika sana, na Kanisa la leo ni dhaifu kwa kuyakosa, ni jambo sahihi kumwomba Mungu ili atuongoze katika hilo, pasipo kujali tunaliitaje na ni theolojia gani tunatumia kulielezea” (“Baptism in the Holy Spirit,” New Dictionary of Theology, uk. 74).

Hitimisho

3

Made with FlippingBook Digital Proposal Maker