Mungu Roho Mtakatifu, Kitabu cha Mwanafunzi, Capstone Module 14 Swahili Student Workbook
/ 1 0 9
M U N G U R O H O M T A K A T I F U
Maswali haya yameandaliwa ili kukusaidia kupitia na kujadili kweli zilizofundishwa kuhusu ubatizo katika Roho Mtakatifu katika sehemu hii ya “Uwepo Wenye Nguvu wa Roho Mtakatifu (Sehemu ya Kwanza).” Tafadhali chukua muda mwingi uwezavyo kujibu maswali haya na mengine ambayo yanatokana na video. Jibu kwa umakini, katika lugha inayoeleweka na kwa ufupi, na inapowezekana, tumia Maandiko kujenga hoja zako! 1. Maandiko wakati mwingine huzungumzia ubatizo katika Roho Mtakatifu kwa kuuhusianisha na uwepo wa Mungu na, wakati mwingine, kwa kuuhusianisha na nguvu za Mungu. Je, ungemjibuje mtu anayeamini kwamba inawezekana kuwa Mkristo lakini bado usiwe na uwepo wa Roho Mtakatifu? 2. Je, unawezaje kueleza ubatizo wa Roho kama tendo la mara moja tu (mtazamo wa makanisa ya Reformed ) ? Ni Maandiko gani yanaweza kusaidia kuunga mkono mtazamo huu? 3. Ni Maandiko gani yanaweza kuunga mkono mtazamo wa ubatizo wa Roho katika hatua nyingi? 4. Je, unaweza kuelezeaje mtazamo wa makanisa ya Holiness juu ya ubatizo wa Roho? 5. Je, unaweza kuelezeaje mtazamo wa Kipentekoste kuhusu ubatizo wa Roho? 6. Je, unaweza kuelezeaje mtazamo wa makanisa ya Pentecostal-Holiness kuhusu ubatizo wa Roho? Somo hili limejitika katika njia ambazo Roho Mtakatifu hutuingiza katika mwili wa Kristo na hututayarisha kufanya kazi kama watu wa Mungu ulimwenguni. ³ Kuzaliwa upya ni kazi ya Roho Mtakatifu inayotufanya “tuzaliwe mara ya pili.” Kupitia kuzaliwa upya, Roho Mtakatifu hubadilisha utu wa ndani wa mtu ili asidhibitiwe tena na asili ya dhambi bali awe na roho mpya kabisa ndani yake ambayo imeumbwa kwa mfano wa Kristo. ³ Kuzaliwa upya ni kipawa cha bure cha Mungu ambacho hakiwezi kupatikana kwa matendo mema au juhudi za kibinadamu. Kama vile uzima ulivyotujia kutoka kwa wazazi wetu bila sisi kufanya chochote kuupata au kuustahili, vivyo hivyo kuzaliwa upya huja kama kipawa cha bure kutoka kwa Mungu ambacho kinaweza kupokelewa tu kwa imani.
Sehemu ya 2
Maswali kwa Wanafunzi na Majibu
3
MUUNGANIKO
Muhtasari wa Dhana Kuu
Made with FlippingBook Digital Proposal Maker