Mungu Roho Mtakatifu, Kitabu cha Mwanafunzi, Capstone Module 14 Swahili Student Workbook
/ 1 1 1
M U N G U R O H O M T A K A T I F U
³ Ni muhimu kwamba tusiyapambanishe kimakosa maandishi ya Paulo kana kwamba yanapingana na yale ya Luka. Badala yake tukubali ushuhuda wote wa Maandiko Matakatifu (vitabu vya Injili, Matendo ya mitume, na Nyaraka), na kutafuta njia za kuzungumza juu ya ubatizo wa Roho kwa namna ambayo tunaweza kusisitiza kuhusu uwepo wake na nguvu zake, kazi yake yote pale tunapopokea wokovu na kazi yake baada ya kuupokea wokovu. Wakristo wanaweza kutokubaliana kuhusu lugha ya kitheolojia inayotumika kuhusiana na suala hili la kuutegemea uwepo na nguvu za Roho Mtakatifu, lakini wote wanapaswa kutafuta kuona kweli hii ikiwa halisi katika maisha yao. Sasa ni wakati wa wewe kujadili pamoja na wanafunzi wenzako maswali yako kuhusiana na huduma ya Roho Mtakatifu ambayo yameibuliwa na somo la leo. Maswali yako ni ya muhimu sana. Mawazo, maswali, na changamoto ulizo nazo sasa lazima ziwekwe mezani na kujadiliwa. Kweli zilizomo katika somo hili kuhusiana na kazi ya Roho Mtakatifu zina maana nyingi kwako, na bila shaka sasa una maswali kuhusu umuhimu wa kweli hizi katika kazi yako Kanisani, na katika maisha na huduma yako. Maswali yafuatayo yanaweza kukusaidia kuunda maswali yako mwenyewe, yaliyo mahususi na muhimu zaidi. * Je, kazi ya Roho ya kuzaa upya (ambayo Maandiko yanarejelea kama kuzaa upya, kufanya upya, kufanya hai, uumbaji mpya) ina maana gani kwa watu waishio katika miji? * Je, kazi ya Roho ya kuwaasili waamini wapya katika familia ya Mungu inapaswa kuathiri vipi namna tunavyofikiri kuhusu Kanisa? Ni maeneo gani yenye nguvu katika Kanisa lako katika utendaji wake kama familia kuhusiana na waamini wapya? Kuna mambo yoyote ambayo yanapaswa kuboreshwa? * Katika kanisa lako, ni wakati gani na jinsi gani mwamini mpya anafundishwa kuhusu kazi ya Roho Mtakatifu ya kuzaa upya na kufanya wana? Ni nini kilikuwa cha faida kubwa kwako katika mchakato huu? Kuna njia ambazo unaweza kuboresha jambo hili? * Je, kanisa lako linaamini nini kuhusu ubatizo katika Roho Mtakatifu? Je, mnashikilia mtazamo wa ubazito kama tendo la mara moja (Hatua moja) au mnaamini katika hatua nyingi? Kwa nini? * Je, tunazuiaje mitazamo yetu tofauti kuhusu ubatizo wa Roho Mtakatifu isiwe kitu ambacho kinampa shetani nafasi ya kusababisha mgawanyiko katika Mwili wa Kristo au kusababisha kundi moja la Wakristo kujisikia wako kiroho zaidi kuliko lingine?
Kutendea kazi somo na matokeo yake kwa mwanafunzi
3
Made with FlippingBook Digital Proposal Maker