Mungu Roho Mtakatifu, Kitabu cha Mwanafunzi, Capstone Module 14 Swahili Student Workbook
1 1 2 /
M U N G U R O H O M T A K A T I F U
MIFANO
Amefanyika mpya kwa kiwango gani?
Hivi majuzi, kupitia huduma ya ushuhudiaji ya Kanisa lako, mwanamume mmoja mwenye umri wa kati na historia mbaya ya kunyanyasa watoto alimpokea Kristo. Anahudhuria kila ibada na anajifunza Maandiko kwa hamu na shauku kubwa kupitia mafunzo ya Biblia ya kikundi na muda wake binafsi wa kujisomea akiwa nyumbani. Ni dhahiri kwamba amekutana naKristo na kwambamabadiliko ya haraka yanatokea katika maisha yake. Amekiri hadharani kuachana na maisha yake ya zamani na amekubali kukutana mara kwa mara na mshirika wa kumfuatilia (aliyepewa jukumu hilo na Mchungaji Kiongozi), ambaye anaweza kumsaidia katika mapambano yake dhidi ya vishawishi na kumwendea na kukiri yale maeneo anayoshindwa. Wakati watu wa kanisa hilo walishangilia alipompokea Kristo, na kufurahi pamoja naye alipokuwa akitoa ushuhuda wake, baadhi ya wazazi wa kanisa hilo hivi karibuni wameanza kueleza wasiwasi wao kuwa huenda mtu huyo ni hatari kwa watoto wao. Jumapili iliyopita kikundi kidogo cha wazazi kilimwendea mchungaji baada ya ibada na kumtahadharisha kwamba ikiwa mtu huyu ataendelea kuhudhuria kanisani, wanadhani watalazimika kuwapeleka watoto wao mahala pengine. Je, mafundisho ya Biblia juu ya kazi ya Roho Mtakatifu ya kuzaa upya na kufanya wana yanapaswa kumuongozaje mchungaji anapozungumza na wazazi na anapotoa huduma ya kichungaji kwa mwongofu huyu mpya na kusanyiko kwa ujumla? Janice amekuwa mkristo kwa miaka miwili hivi. Amekuwa mshirika mwaminifu katika ibada kanisani ambaye “amezama” katikamafundisho yaBiblia yanayotolewa kupitia mahubiri na vipindi vya kujifunza Biblia. Kila muumini anayemfahamu anakubali kwamba Janice ni mkristo anayekua kwa kasi na anayempenda Yesu na anataka kumtumikia kwa uaminifu. Hivi majuzi alikuwa akisoma Kitabu cha Matendo ya Mitume na akakutana na swali la Paulo kwa wanafunzi wa Efeso katika ile sura ya 19, “Je, mlipokea Roho Mtakatifu mlipoamini?” Anakuja kwako na ni dhahiri kwamba swali hilo limemchanganya. Anasema, “Ninajua kwamba Mungu aliingia ndani yangu miaka miwili iliyopita na kubadilisha maisha yangu. Siku zote nimekuwa nikidhani hiyo ilikuwa kazi ya Roho Mtakatifu lakini sasa sina uhakika sana. Je, nilipokea Roho Mtakatifu nilipoamini? Kuna kitu kingine cha tofauti kuhusu Roho Mtakatifu ambacho ninahitaji kukipata? Sijui hata cha kufikiria!” Utamwambia nini? Kwa nini? Sijui hata cha kufikiria !
1
3
2
Roho Mtakatifu wa Mungu ndiye anayetuzaa upya (kutufanya wapya) na kutufanya wana katika familia ya Mungu. Kubatizwa (kuzamishwa) katika Roho wa Mungu hutuunganisha na Kristo na Kanisa lake na pia hutuwezesha kupokea
Marejeo ya Tasnifu ya Somo
Made with FlippingBook Digital Proposal Maker