Mungu Roho Mtakatifu, Kitabu cha Mwanafunzi, Capstone Module 14 Swahili Student Workbook

/ 1 1 3

M U N G U R O H O M T A K A T I F U

nguvu za Mungu kwa ajili ya kuishi maisha matakatifu na kushuhudia. Wakristo wanatofautiana kuhusu endapo Roho Mtakatifu anapokelewa kwa ukamilifu wakati wa kuokoka (mtazamo wa makanisa ya Reformed ) au kama tukio tofauti la ujazo wa Roho Mtakatifu linapaswa kutokea baada ya kuokoka kwa kusudi la kumpa mwamini nguvu zaidi (mitazamo ya makanisa ya Holiness na ya Kipentekoste). Ikiwa una nia ya kusoma zaidi kuhusiana na kazi ya Roho Mtakatifu katika maisha ya Kanisa na mwamini binafsi, unaweza kujaribu vitabu hivi: Fee, Gordon. Paul, the Spirit, and the People of God. Peabody, MA: Hendrickson, 1996. Graham, Billy. The Holy Spirit: Activating God’s Power in Your Life. Dallas, TX: Word Publishing, 1997. Green, Michael. I Believe in the Holy Spirit. Grand Rapids, MI: Wm. B. Eerdmans, 1975. Kiini cha mafundisho haya ni ili uweze kutafuta kuhusianisha kweli hizi na huduma yako mwenyewe kupitia kanisa lako. Jinsi Mungu anavyoweza kukutaka ubadilike au ubadilishe mbinu yako ya huduma kulingana na kweli hizi inategemea sana uwezo wako wa kusikia kile ambacho Roho Mtakatifu anakuambia kuhusu mahali ulipo, mahali uongozi wako wa kichungaji ulipo, mahali washirika wa kanisa lako walipo, na kile hasa ambacho Mungu anakuitia kufanya sasa hivi kuhusu kweli hizi, kama kipo. Panga kutumia muda mzuri wiki hii kutafakari kazi ya Roho Mtakatifu katika maisha ya mwamini. Unapofikiria na kujipanga kwa ajili ya kazi yako ya huduma ili kukamilisha moduli hii, unaweza kuitumia kuzitendea kazi kweli hizi kwa njia ya vitendo. Utafute uso wa Mungu kwa ajili ya ufahamu zaidi, na urudi wiki ijayo ukiwa tayari kuwashirikisha wanafunzi wengine katika darasa lako maarifa ambayo umeyapata. Labda kuna baadhi ya mahitaji maalum au maswali mahususi ambayo Roho Mtakatifu ameyakazia kupitia kujifunza kwako na majadiliano ya somo hili juu ya Roho Mtakatifu. Usisite kutafuta mtu wa kushirikiana naye katika maombi ambaye anaweza kushiriki kubeba mzigo ulionao na kuinua maombi yako mbele za Mungu. Bila shaka, Mkufunzi wako yuko tayari sana kutembea nawe katika hili, na viongozi wako wa kanisa, hasa mchungaji wako, wanaweza kuwa na ujuzi maalum wa kukusaidia kujibu maswali yoyote magumu yanayotokana na kutafakari kwako juu ya somo hili. Kuwa wazi kwa Mungu na umruhusu akuongoze jinsi anavyotaka.

Nyenzo na Bibliografia

3

Kuhusianisha somo na huduma

Ushauri na Maombi

Made with FlippingBook Digital Proposal Maker