Mungu Roho Mtakatifu, Kitabu cha Mwanafunzi, Capstone Module 14 Swahili Student Workbook

/ 1 2 1

M U N G U R O H O M T A K A T I F U

b. Warumi 12:4-8 – Kwa kuwa kama vile katika mwili mmoja tuna viungo vingi, wala viungo vyote havitendi kazi moja; 5 Vivyo hivyo na sisi tulio wengi tu mwili mmoja katika Kristo, na viungo, kila mmoja kwa mwenzake. 6 Basi kwa kuwa tuna karama zilizo mbalimbali, kwa kadiri ya neema mliyopewa; ikiwa unabii, tutoe unabii kwa kadiri ya imani; 7 ikiwa huduma, tuwemo katika huduma yetu; mwenye kufundisha, katika kufundisha kwake; 8 mwenye kuonya, katika kuonya kwake; mwenye kukirimu, kwa moyo mweupe; mwenye kusimamia kwa bidii mwenye kurehemu, kwa furaha.

c. 1 Petro 4:10 - kila mmoja kwa kadiri alivyoipokea karama, itumieni kwa kuhudumiana; kama mawakili wema wa neema mbalimbali za Mungu.

d. 1 Wakorinhto 12:4-6 - Basi pana tofauti za karama; bali Roho ni yeye yule. 5 Tena pana tofauti za huduma, na Bwana ni yeye yule. 6 Kisha pana tofauti za kutenda kazi, bali Mungu ni yeye yule azitendaye kazi zote katika wote..

4

Neno Pneumatikos , ambalo ni kivumishi kinachotokana na nomino, pneuma, hutoa maana ya kitu cha ulimwengu wa roho/Roho, cha asili ya roho/ Roho, kinachoakisi au kinachowakilisha roho/Roho…. Kama nomino isiyoonyesha jinsi, ~a kiroho, mambo ya rohoni. ~ “Roho.” The New International Dictionary of New Testament Theology , Vol. 3. Colin Brown, ed. Grand Rapids: Zondervan, 1986. uk. 706-707.

2. Neno Pneumatikos : Roho wa Mungu akiwa dhahiri ndani yetu na kupitia sisi.

a. 1 Wakorintho 12:1 – Basi, ndugu zangu, kwa habari ya karama za roho [ pneumatikoon ], sitaki mkose kufahamu.

b. 1 Wakorintho 12:7 – Lakini kila mmoja hupewa ufunuo wa Roho kwa kufaidiana.

c. Ingawa katika Kiswahili (na hata katika Kiingereza), mstari wa kwanza unazungumzia kuhusu karama za rohoni, neno linalotafsiriwa kama karama kimsingi halipo katika lugha ya asili ya andiko hili. Neno linalopatikana katika lugha ya asili ya andiko husika lingefaa zaidi kutafsiriwa kama “mambo ya kiroho” (Basi

Made with FlippingBook Digital Proposal Maker