Mungu Roho Mtakatifu, Kitabu cha Mwanafunzi, Capstone Module 14 Swahili Student Workbook
1 2 2 /
M U N G U R O H O M T A K A T I F U
ndugu zangu kwa habari ya “mambo ya rohoni,” sitaki mkose kufahamu). Kwa hiyo anajaribu kusema nini hapa? Kama tukiendelea kusoma mpaka 1 Kor. 12:7, mstari huo unatusaidia kuelewa vizuri zaidi kile ambacho Paulo anamaanisha kwa kusema “mammbo ya rohoni”: “Lakini kila mmoja hupewa ufunuo wa Roho kwa kufaidiana.” Ufunuo una maanisha kwamba kitu fulani kimewekwa wazi na dhahiri. Kwa maneno mengine tunaweza kuongelea karama za rohoni, sio tu kama aina fulani mahususi ya uwezo ambao mtu anapewa na Mungu kwa ajili ya huduma, lakini pia kama kitu chochote ambacho kinafanya uwepo na nguvu za Roho Mtakatifu kuwa dhahiri au kujulikana. Hivyo basi, tafsiri bora zaidi ya mstari wa kwanza kwa Kiswahili ingeweza kueleweka zaidi kwa kuandikwa kama ifuatavyo: “Basi, ndugu zangu, kwa habari ya madhihirisho ya Roho , sitaki mkose kufahamu.”
3. Kuelekea ufafanuzi wa karama za rohoni
a. “Kitu chochote, tukio lolote, au mtu yeyote anayetumika kama chombo cha Roho, au anayemdhihirisha Roho, au anayeakisi utendaji wa Roho, huyo ni karama ya rohoni” ( Baker Encyclopedia of the Bible ) .
4
b. “Karama ni uwezo unaotolewa na Roho kwa ajili ya huduma ya Kikristo” (Leslie B. Flynn, 19 Gifts of the Spirit ) .
c. “Karama ya rohoni ni karama ya neema ya kiungu ambayo inathibitishwa na uwezo fulani ambao unaufaidia mwili wa Kristo.” (Thomas C. Oden, Life in the Spirit ).
4. Katika maana na tafsiri zote, kusudi la karama za rohoni ni kuliwezesha Kanisa kukamilisha kusudi lake ulimwenguni. Kwa sabau hiyo, karama za rohoni zipo ili “kufaidiana” (1 Kor. 12:7) badala ya kutumika kwa faida ya mtu binafsi.
Made with FlippingBook Digital Proposal Maker