Mungu Roho Mtakatifu, Kitabu cha Mwanafunzi, Capstone Module 14 Swahili Student Workbook

/ 1 2 3

M U N G U R O H O M T A K A T I F U

C. “Kuna karama ngapi za rohoni?” na “Karama hizo ni zipi?”

1. Vifungu muhimu kwa ajili ya kujifunza karama za rohoni: kila moja ya sura hizi inajumuisha mifano ya baadhi ya karama za rohoni na maagizo ya jinsi zinavyopaswa kutumika katika Kanisa la Mungu.

a. Warumi 12

b. 1 Warumi 12

c. Waefeso 4

d. 1 Petro 4

2. Karama zisizo na idadi: kuna idadi isiyoweza kuhesabika ya namna ambazo neema ya Mungu inaweza kufanya kazi kupitia sisi na namna ambazo Roho wa Mungu anaweza kujidhihirisha ndani yetu.

4

Watu wengi wamejaribu kutengeneza orodha ya karama za rohoni zilizomo katika Agano Jipya. Jambo hili mara nyingi limesababisha kutokubaliana kwa sababu kila orodha, katika sura nne kuu zinazoelezea karama, ni tofauti na wakati mwingine karama moja inaonekana kuitwa kwa majina tofauti. Kwa hiyo mtu akiuliza kuna karama ngapi za rohoni, nitamwambia kwamba haulizi swali sahihi. Kwa kuwa chochote anachofanya Roho Mtakatifu ili kufanya nguvu na uwepo wake kuonekana katika maisha ya waamini ni karama ya rohoni (udhihirisho), kuna uwezekano wa idadi isiyo na kikomo ya njia ambazo Roho Mtakatifu anaweza kuwapa watu karama kwa ajili ya huduma. Hata hivyo, inaonekana wazi kwamba, kwa mujibu wa Biblia, angalau karama zile mahususi ambazo zimetajwa katika Maandiko zitakuwepo katika Kanisa (ingawa inawezekana kusiwepo na kila karama katika kila kusanyiko) na kwamba karama hizi zitatumika kama msingi wa kuelewa jinsi Mungu anavyoliwezesha Kanisa lake kutenda kazi yake.

Haiwezekani kabisa kutaja idadi ya karama ambazo Kanisa duniani kote limezipokea toka kwa Mungu, katika jina la Yesu Kristo... ~ Irenaeus alinukuliwa katika A Dictionary of Early Christian Beliefs . David W. Bercot, ed. Peabody, MA: Henrickson, 1998. uk. 299.

Made with FlippingBook Digital Proposal Maker