Mungu Roho Mtakatifu, Kitabu cha Mwanafunzi, Capstone Module 14 Swahili Student Workbook

1 3 4 /

M U N G U R O H O M T A K A T I F U

I. Roho Anayetakasa

Muhtasari wa Sehemu ya 2 ya Video

A. Kuelewa maana ya utakaso katika Maandiko

1. Ufafanuzi

a. Kwa Kiebrania: q ā daš; Kwa Kiyunani: hagiaz ō Katika Maandiko, neno “kutakasa” kiuhalisia linamaanisha “kuweka kando kwa ajili ya matumizi matakatifu.” Kitu chochote ambacho kilitengwa kwa ajili ya Mungu kilitakaswa.

b. Kimantiki “kutakasa” kuna maana: kufanya kitu kiwe kitakatifu (paispo chochote chenye kuharibu, kutia unajisi, au kuondoa ukamilifu), kisafi na kisicho na mawaa.

2. Mifano ya KiMaandiko:

4

a. Hema na samani zake (Kut. 40:9)

b. Wanyama kwa ajili ya dhabihu (Law. 22:21)

c. Taifa zima la Israel (Law. 11:44)

d. Kanisa la Agano Jipya (1 Kor. 1:2; 2 Kor. 6:16-18, 7:1)

Made with FlippingBook Digital Proposal Maker