Mungu Roho Mtakatifu, Kitabu cha Mwanafunzi, Capstone Module 14 Swahili Student Workbook
/ 1 3 3
M U N G U R O H O M T A K A T I F U
5. Kuna uhusiano gani kati ya karama za rohoni na kukomaa kiroho? 6. Ni kwa namna gani watu wanaweza kutambua aina ya karama za rohoni walizonazo? 7. Kwa nini ni muhimu kwa wachungaji kutambua karama za rohoni walizonazo washirika katika mikusanyiko yao? 8. Ni kwa namna gani Hema la Kukutania linatusaidia sisi kuelewa namna Roho Mtakatifu anakaa ndani yetu? 9. Neno la Kiyunani Paraclete linamaanisha nini? Linatusaidiaje kuielewa kazi ya Roho Mtakatifu ya kukaa ndani yetu? 10. Angalia kwa ufupi Warumi 8. Je, ni huduma zipi za Roho Mtakatifu anayekaa ndani yetu zimeelezewa katika kifungu hiki?
Uwepo Wenye Nguvu wa Roho Mtakatifu (Sehemu ya Pili) Sehemu ya 2: Roho Anayetia Muhuri na Kutakasa
Mch. Terry G. Cornett
4
Katika sehemu hii tutaangalia kazi ya Roho Mtakatifu katika kuwatia muhuri na kuwatakasa wale walio wa Kristo Yesu. Lengo letu la sehemu hii, Roho Anayetia Muhuri na Kutakasa , ni kukuwezesha kuona kwamba: • Roho wa Mungu ndiye anayetubadilisha hata tumfananie Kristo. • Utakaso una sehemu ya zamani, ya sasa na ya baadaye. • Roho wa Mungu yuko vitani dhidi ya uovu. • Tunda la Roho ni viashiria muhimu vya kuzalishwa kwa maisha ya Kristo ndani yetu. • Huduma ya Roho ya kutia muhuri hutupatia uhakikisho wa wokovu wetu.
Muhtasari wa Sehemu ya 2
Made with FlippingBook Digital Proposal Maker