Mungu Roho Mtakatifu, Kitabu cha Mwanafunzi, Capstone Module 14 Swahili Student Workbook

1 3 6 /

M U N G U R O H O M T A K A T I F U

katika Agano Jipya ni “ukuaji katika utakatifu ambao unapaswa kufuata baada ya kuongoka.” (3) Dhumuni [kukamilishwa] - KUTUKUZWA (a) Warumi 8:18; 1 Yohana 3:2 (b) Z INGATIA: Lengo kuu na la mwisho la wokovu wetu ni kwamba tutakuwa na mwili, nafsi, na roho mpya ambayo imewekwa huru kabisa dhidi ya dhambi, magonjwa, na kifo, na tutaishi katika ulimwengu mpya ambamo Mungu atakuwa Mfalme na haki itatawala.

Kama ilivyo kwa habari ya ubatizo

wa Roho Mtakatifu, fundisho la utakaso pia limekuwa chanzo cha mabishano miongoni mwa Wakristo. Rejelea kiambatisho kwa ajili ya taarifa zaidi.

b. Lengo la utakaso wote ni kufanana na Kristo. (1) Warumi 8:29-30 (2) 1 Yohana 2:1-6

(3) [Utakaso ni] kazi ya neema ya Mungu itolewayo bure, ambayo kwayo tunafanywa upya katika utu wetu wote ili tuweze kufanana na Mungu, na tunawezeshwa zaidi na zaidi kufa kwa habari ya dhambi na kuishi katika haki. ( The Westminister Catechism ) . B. Kazi ya Roho katika utakaso Japo kuwa tu wenye dhambi, Mungu anafanya maisha matakatifu ya Kristo kuwa mbadala wa maisha yetu. Maisha ya Kristo yasiyo na dhambi na kifo chake kama dhabihu ya dhambi viliwaheshabia haki wote walioamini. Utakatifu wa Kristo umefanyika mbadala wa udhambi wao. Huku ni kuhesabiwa utakatifu (kuhesabiwa haki). Roho ndiye atupaye shauku ya kuwa watakatifu na nguvu ya kuishi maisha matakatifu.

4

1. Roho Mtakatifu yuko katika mapambano na uovu

a. Kiulimwengu : Kila mahali ulimwenguni ambapo watu wameasi utawala na utunzaji mzuri wa Mungu, Roho anafanya kazi ya kurejesha mambo na kuyarekebisha tena.

Made with FlippingBook Digital Proposal Maker