Mungu Roho Mtakatifu, Kitabu cha Mwanafunzi, Capstone Module 14 Swahili Student Workbook

/ 1 3 7

M U N G U R O H O M T A K A T I F U

b. Kibinafsi: Roho anapigana vita na asili ya dhambi inayoishi ndani ya kila mtu, Gal. 5:17.

Paulo anatoa ushauri kuhusu kushinda vita dhidi ya dhambi. Anasema: “Tukiishi kwa Roho, na tuenende kwa Roho.” Neno linalotafsiriwa kama “kushika hatua,” (au “kutembea” katika baadhi ya matoleo), kwa hakika ni neno la kijeshi [stoicheo] ambalo linatoa taswira ya askari wanaofuatana na afisa mkuu wanapoandamana kwenda vitani.

c. Kazi ya utakaso inaonyeshwa katika lugha na mapambano ya kijeshi. (1) Vaeni “silaha zote za Mungu” na “ipokeeni chapeo ya wokovu, na upanga wa Roho, ambao ni neno la Mungu, mkisali kila wakati katika Roho, kwa sala zote na maombi,” Efe. 6. (2) Wakolosai 3:5 d. Tunaishi “katikati ya nyakati”: ambapo utakaso ni jambo ambalo “tayari limetokea” na pia “bado halijatokea.” (1) Ukweli: tumetakaswa na hakuna haja ya kutenda dhambi, 1 Yoh 2:1a. (2) Ukweli: Wakristo hutenda dhambi na wanahitaji msamaha, 1 Yoh. 2:1b.

(3) Ukweli: tumetakaswa tayari, Ebr. 10:14a. (4) Ukweli: bado tunatakaswa, Ebr. 10:14b. (5) Wafilipi 3:12-16

4

2. Matokeo ya uwepo wa Roho Mtakatifu ndani ya mwamini ni maisha matakatifu. a. Roho hafanyi kazi tu kupinga dhambi kwa bidii bali pia kuzalisha hali ya kufanana na Kristo kikamilifu.

b. Tunda la Roho kama kipimo kikuu cha kufanana na Kristo. (1) Wagalatia 5:22-24

(2) Neno lililotafsiriwa kama “tunda” hapa liko katika umoja katika lugha ya Kiyunani. Hakuna matunda tofauti ya Roho Mtakatifu kwa ajili yetu sisi kuokota au kuchagua miongoni mwa hayo mengi. Pale ambapo Roho Mtakatifu anafanya kazi yake ya kutakasa, basi vitu vyote hivi vitatokea.

Made with FlippingBook Digital Proposal Maker