Mungu Roho Mtakatifu, Kitabu cha Mwanafunzi, Capstone Module 14 Swahili Student Workbook

1 3 8 /

M U N G U R O H O M T A K A T I F U

C. Kanuni za msingi za kitheolojia kuhusiana na utakaso.

1. Utakaso unategemea kazi ya Kristo ya Kalvari lakini unafanywa kwa kila mwamini kibinafsi kupitia kazi ya Roho Mtakatifu.

a. Kile ambacho Kristo alikifanya kwa ajili yetu msalabani ndio msingi wa kile ambacho Roho Mtakatifu anaendelea kukifanya ndani yetu sasa. Imani katika Kristo ndio chanzo cha kuhesabiwa haki na utakaso. (1) Waebrania 10:14 (2) Warumi 3:24 b. Tunapoweka imani yetu katika Kristo, Roho Mtakatifu ndiye anayekuja kwetu ili kutufanya tuwe kama Yeye [Kristo]. Roho ni sehemu ya Uungu Mtakatifu inayotufanya tugeuzwe kuwa watu wenye haki. (1) 1 Wakorintho 6:9-11 (ling. 1 The. 4:7-8) (2) Warumi 15:16

4

2. Kazi ya Roho ndani yetu mara zote inazalisha chuki dhidi ya dhambi na kuongeza utakatifu wa maisha ya mtu. Hakuna Mkristo yeyote anayepaswa kuikubali dhambi kuwa ni jambo la kawaida au kwamba haiepukiki.

a. Maandiko yanaamrisha utakatifu wa maisha (Kut. 19:6; Yoh. 5:14; 1 Pet. 1:15-16). Mungu asingeamuru kitu ambacho hakiwezekani au kitu ambacho hangekitarajia.

b. Maandiko yanaahidi utakatifu wa maisha kama sehemu ya wokovu wa Mungu (Kum. 30:6; Eze. 36:25-27, Mt. 5:6; 1 Thes. 5:23-24). Mungu asingeahidi kitu ambacho hakukusudia kukifanya.

Made with FlippingBook Digital Proposal Maker