Mungu Roho Mtakatifu, Kitabu cha Mwanafunzi, Capstone Module 14 Swahili Student Workbook
/ 1 3 9
M U N G U R O H O M T A K A T I F U
3. Usikate tamaa kamwe juu ya uwezo na utayari wa Roho wa kuwafanya Wakristo kuwa watakatifu.
a. Huruma ya Kristo kwa wenye dhambi (Mt. 18:21-22; 1 Yoh. 2:1) daima inapaswa kuwekwa mbele katika akili zetu. Roho Mtakatifu anakuja kwetu kama Roho wa Yesu (Yoh. 14:16-18; Flp. 1:19 ) ambaye ni “rafiki wa wenye dhambi”.
b. Roho yupo ili kutujaza tena na tena ili kila wakati tuweze kuanza upya tukiwa na nguvu mpya katika vita yetu dhidi ya dhambi. (1) Waefeso 5:18 - “Mjazwe Roho” (2) Kitenzi hiki “mjazwe” kiko katika wakati uliopo wa shuruti, (shuruti hapa inamaanisha hiyo ni amri). Wakati uliopo katika Kiyunani hutumika kuonyesha kitendo kinachoendelea au kinachorudiwa tena na tena.
Mtu awaye yote asije akajisifu kwamba yeye hana hatia–huyo na aangamie zaidi kwa kujikweza— anaelekezwa na kufundishwa kwamba anatenda dhambi kila siku. Maana anaambiwa aombe kila siku kwa ajili ya dhambi zake. ~ Cyprian quoted in A Dictionary of Early Christian Beliefs . David W. Bercot, ed. Peabody, MA: Hendrickson, 1998. uk. 618.
4. Mkristo aliyekomaa hatategemea ushindi wa wakati uliopita bali ataendelea kuwa macho daima dhidi ya dhambi.
4
a. Hakuna hali yoyote ambayo katika hiyo mkristo anaweza kudai kihalali kwamba amevuka tayari na kuwa mbali na uwezekano wa kutenda dhambi. Katika Mtaguso wa Carthage (Mwaka 418 B.K), Kanisa lilipinga mtazamo wa kwamba wakristo hawatendi dhambi. Mababa hao wa kale wa Kanisa walisisitiza kwamba maombi yanayopatikana katika Sala ya Bwana “Utusamehe makosa yetu” na “Usitutie majaribuni” ni maombi ambayo wakristo wote wanahitaji kuomba. Walitoa sababu kwamba kama hii ni sala ya wanafunzi wote, basi hakuna mkristo anayeweza kudai kwamba yeye yuko juu sana katika utakatifu kiasi kwamba hawezi kabisa kupata majaribu wala kutenda dhambi.
Made with FlippingBook Digital Proposal Maker