Mungu Roho Mtakatifu, Kitabu cha Mwanafunzi, Capstone Module 14 Swahili Student Workbook

1 4 4 /

M U N G U R O H O M T A K A T I F U

Hitimisho

» Roho ndiye anaye “watakasa na kuwatia muhuri” wale wanaoweka imani yao katika Yesu kama Bwana na Kristo. » Katika kazi yake ya utakaso, Roho anatumia ushindi wa Kristo dhidi ya dhambi uliopatikana msalabani katika maisha ya kila mwamini ili kumwezesha kuishi maisha matakatifu. » Roho anatenda kazi ulimwenguni kupigana na uovu na kuzaa matunda ya haki. » Ingawa tunaishi katika ulimwengu ambao uovu bado hauja ondolewa na siku ya mwisho ya hukumu ya Mungu, Roho Mtakatifu amewatia muhuri wale ambao wameweka imani yao katika Kristo Yesu ili kwamba waweze kufahamu wanamilikiwa na Mungu, wawe na uhakika wa uwepo wake, na watambue kwamba wanalindwa na Yeye wakati wote wa zama hizi za uovu. Maswali yafuatayo yameandaliwa ili kukusaidia kupitia maelezo yaliyopo katika sehemu ya pili ya video. Hapa pia unaweza tena ukahitaji kuanza kwa kuangalia kwanza akrostiki ya RABBIS . Jibu kwa uwazi na kwa ufupi, na inapowezekana tumia Maandiko kujenga hoja zako. 1. Neno “kutakasa”lina maana gani? 2. Kuna kufanana na tofauti gani kati ya kuhesabiwa haki, kutakaswa na kutukuzwa? 3. Utamshauri vipi mtu ambaye anadai kuwa ameokoka lakini hajaonyesha ushahidi wa tunda la Roho? 4. Je, kuna hatari zozote katika “kujitahidi kufikia ukamilifu”? Ikiwa ndivyo, ni hatari zipi? Je, kuna hatari zozote za “kutojitahidi kufikia ukamilifu”? Ikiwa ndivyo, ni hatari zipi? 5. Ni kwa namna gani sitiari ya muhuri wa nta wa kale wa dola ya Kirumi ( sphragis ) , inasaidia katika kuelewa kile ambacho Roho Mtakatifu anafanya katika maisha ya waamini? 6. “Ushuhuda wa Roho” ni nini?

Sehemu ya 2

4

Maswali ya Wanafunzi na Majibu

Made with FlippingBook Digital Proposal Maker