Mungu Roho Mtakatifu, Kitabu cha Mwanafunzi, Capstone Module 14 Swahili Student Workbook
/ 1 4 3
M U N G U R O H O M T A K A T I F U
Mungu, ajuaye mioyo ya watu, akawashuhudia, akiwapa Roho Mtakatifu vile vile kama alivyotupa sisi,” Mdo 15:8. (2) Kwa maana watendao kazi vyema hujipatia daraja nzuri, na ujasiri mwingi katika imani iliyo katika Kristo Yesu, 1 Tim. 3:13. c. Kupitia nyakati za mashaka na kujihoji ikiwa kweli tumeokolewa haimaanishi kwamba hatuna ushuhuda wa Roho. (1) 1 Yohana 3:19-20 (2) Dhamiri ya uhakika na ufahamu wa kina juu ya dhambi, hatia, na kukosa utoshelevu ni ishara ya kazi ya Roho. Mtu mwenye “dhamiri sugu” (1 Tim. 4:1-2) au mwenye “kujikweza kwa utoshelevu wake wenyewe” (Luka 18:11; Yohana 9:41) ndiye anayepaswa kuhangaika kwa habari ya uhusiano wake na Mungu. Msukumo wa kichungaji siku zote ni “kuwafariji waliohuzunishwa” na “kuwahuzunisha wanaojifariji.”
3. Kutiwa muhuri hutukumbusha kwamba wokovu wetu ni wa wakati ujao na wa sasa.
4
a. Na amemuweka Roho katika mioyo yetu kama amana [arabuni], dhamana ya mambo yajayo, 2 Kor. 1:21-22
b. Ambaye kwa yeye mlitiwa muhuri hata siku ya ukombozi, Efe. 4:30
c. Sisi tunaookolewa, 1 Kor. 1:18 (linganisha na 2 Kor. 2:15).
d. Mpaka “siku ya Bwana” Yesu atakaporudi kuhukumu ulimwengu; kushinda dhambi, mauti na kuzimu; kutupatia miili mipya, na kuumba upya mbingu na nchi, lazima tuishi kwa imani na tumaini kuliko kuishi kwa kuona na kwa uzoefu. Roho Mtakatifu anatuwezesha kuonja nguvu ya “wakati ujao” (Ebr. 6:5) na kazi yake katika maisha yetu ni aina ya mazao ya kwanza (malimbuko) ambayo yanatuhakikishia mavuno yajayo.
Made with FlippingBook Digital Proposal Maker