Mungu Roho Mtakatifu, Kitabu cha Mwanafunzi, Capstone Module 14 Swahili Student Workbook

1 4 2 /

M U N G U R O H O M T A K A T I F U

b. Uwepo wa Mungu unazungumza nasi (ushuhuda wa Roho). (1) Roho anatupa Maandiko ambayo hutengeneza msingi wa ujasiri wetu (ushuhuda kutoka nje), 1 Yohana 5:13. (2) Roho huzungumza na roho zetu ili kutuhakikishia kwamba tunamilikwa na Mungu (ushuhuda kutoka ndani). (a) Warumi 8:16 (linganisha na 1 Yoh. 3:24; Mdo 15:8)

(b) Wagalatia 4:6-7 (c) 1 Yohana 3:24

2. “Ushuhuda wa Roho”

a. “Ushuhuda wa Roho” ni kazi ya Roho Mtakatifu inayompa mwamini ufahamu wa wazi kwamba amepatanishwa na Mungu. (1) Ni maarifa ya ndani na ya kibinafsi ambayo yanaambatana na maarifa yatokayo nje katika Neno. (2) Ushuhuda wa Roho ni msukumo wa ndani ya nafsi, ambapo Roho wa Mungu huishuhudia moja kwa moja roho yangu kwamba mimi ni mtoto wa Mungu, kwamba Yesu Kristo amenipenda, na kujitoa kwa ajili yangu; na kwamba dhambi zangu zote zimefutwa, na mimi, hata mimi, nimepatanishwa na Mungu (John Wesley [Mwanzilishi wa Umethodisti]). b. Roho vilevile anatushuhudia kupitia uzoefu wetu wa kila siku pamoja na Mungu baada ya kuokoka. Matukio (ambayo Mungu ametenda katika maisha yetu kwa nguvu) hutusaidia kukumbuka na kuwa na uhakika wa uwepo wake kwa namna endelevu maishani mwetu. (1) Hivyo uhakikisho huo hauji tu kupitia sauti ya ndani ya Roho lakini pia kupitia kazi yake inayoonekana dhahiri katika maisha yetu. Wakati akida wa Kirumi Kornelio alipomkubali Kristo yeye na nyumba yake walipata karama za lugha zilizotolewa na Roho Mtakatifu. Petro anapolitafakari tukio lile alisema: “Na

4

Made with FlippingBook Digital Proposal Maker