Mungu Roho Mtakatifu, Kitabu cha Mwanafunzi, Capstone Module 14 Swahili Student Workbook

1 5 0 /

M U N G U R O H O M T A K A T I F U

kani tu bali ni nafsi ya kiungu ambayo huwaongoza na kuwafundisha watu wa Mungu. Tumekumbushwa kwamba yeye ndiye chanzo cha ufunuo wa kiunabii na njia ambayo kwayo Maandiko yaliyovuviwa yalitujia. Pia tuliona kwamba yeye ndiye anayeuhakikisha ulimwengu kwa habari ya dhambi na kwamba haiwezekani kuitambua Kweli na kuijia bila kuvutwa kupitia kazi ya Roho Mtakatifu. Hatimaye, tulitumia akrostiki ya RABBIS kujikumbusha kazi kuu za Roho katika maisha ya mwamini (Kuzaa Upya, Kuasili yaani kufanya wana, Ubatizo, Utoaji wa Karama, Kukaa ndani ya mwamini, Kutia Muhuri, na Kutakasa). Pengine muhtasari bora zaidi wa kozi hii ni huu kutoka kwa Mtakatifu Basil (329 379 BK): Kwa njia ya Roho Mtakatifu huja urejesho wetu katika paradiso, kupaa kwetu katika ufalme wa mbinguni, kurudi kwetu kufanywa wana, uhuru wetu wa kumwita Mungu Baba yetu, kufanyika kwetu washiriki wa neema ya Kristo, kuitwa kwetu wana wa nuru, kushiriki kwetu katika utukufu wa milele na katika neno, kuletwa kwetu katika hali ya “ukamilifu wa baraka, katika ulimwengu huu na ule ujao, wa vipawa vyote vyema vilivyowekwa kwa ajili yetu, kwa ahadi yake, kwa njia ya imani, tukitazama mwonekano wa neema yake kana kwamba tayari vipo, tunaingojea furaha kamili. ~ St. Basil. On the Holy Spirit. Sura ya. 15.

4

Made with FlippingBook Digital Proposal Maker