Mungu Roho Mtakatifu, Kitabu cha Mwanafunzi, Capstone Module 14 Swahili Student Workbook
/ 1 7 1
M U N G U R O H O M T A K A T I F U
Mila (muendelezo)
Mungu alifunua kazi yake ya wokovu kwa wale ambao walitoa ushuhuda wao kwa kuona utukufu wake, kwanza katika Israeli, na kisha zaidi sana katika Yesu Kristo Masihi. Ushuhuda huu ni wa lazima kwa watu wote, kwa wakati wote, na kwa mahali popote, ni mapokeo yenye mamlaka ambayo kwayo mapokeo yote yanayofuata yanahukumiwa.
2. Mapokeo Makuu: Mitaguso ya Kiekumene na Imani Zao 2
2 Tazama kiambatisho B, “Kufafanua Mapoleo Makuu,”
Kile ambacho kimeaminiwa kila mahali, siku zote, na kwa watu wote.
mwishoni mwa maelezo haya.
~ Vincent of Lerins
Mapokeo Makuu ndiyo mafundisho ya msingi (doktrini) ya Kanisa. Yanawakilisha fundisho la Kanisa kama lilivyoelewa Mapokeo Yenye Mamlaka (Maandiko Matakatifu), na kuweka katika muhtasari zile kweli za msingi ambazo wakristo wote wa nyakati zote wamezikiri na kuziamini. Kanisa zima (la Katoliki, Othodoksi na Protestanti) linakubaliana na matamko haya ya kimafundisho. Ibada na theolojia za Kanisa zinaakisi fundisho la msingi, ambalo linaleta ujumla wake na kutimizwa katika nafsi na kazi za Yesu Kristo. Kutoka nyakati za Kale, wakristo wameonyesha kujitolea kwao kwa Mungu kupitia Kalenda ya Kanisa, na mpangilio wa Ibada wa mwaka ambao unajumuisha na kuyaendeleza matukio ya maisha ya Kristo. 3. Mapokeo Maalum ya Kanisa: Waanzilishi wa Madhehebu na Taratibu mbalimbali Kanisa la Wapresbiteri la Marekani lina washrika takriban milioni 2.5, makusanyiko 11,200 na wahudumu walioapishwa 21,000. Wapresbiteri wanafuatilia historia yao hadi karne ya 16 na Matengenezo ya Kiprostanti. Urithi wetu na mengi ya yale tunayo yaamini, yalianza na mwanasheria Mfaransa aitwaye John Calvin (1509-1564), ambaye uandishi wake ulikazia sana juu ya fikra za Matengenezo ambazo zilikuja kabla yake. ~ Kanisa la Wapresbiteri, Marekani. Wakristo wameonyesha imani yao kwa Yesu Kristo katika njia mbalimbali kupitia harakati na mapokeo mahususi ambayo yanakumbatia na kuelezea Mapokeo Yenye Mamlaka na Mapokeo Makuu kwa namna za kipekee. Kwa mfano, vuguvugu za Kikatoliki zimetokeo nyakati za watu kama Benedict,
3 Hata mrengo wenye msimamo mkali zaidi wa Matengezezo ya Kiprotestanti (Wanabaptisti) ambao walikuwa wenye kusitasita zaidi kushikilia Kanuni za Imani kama maelekezo ya msingi ya imani, bado walikubaliana na yale yaliyokuwa yameandikwa mle. “Walikubali Imani ya Kitume - waliiita ‘Imani,’ Der Glaube, kama walivyofanya watu wengine wengi.” Mtazame Mwanatheolojia John Howard Yoder, Preface to Theology: Christology and Theological Method. Grand Rapids: Brazos
Press, 2002. k. 222-223.
Made with FlippingBook Digital Proposal Maker