Mungu Roho Mtakatifu, Kitabu cha Mwanafunzi, Capstone Module 14 Swahili Student Workbook
1 7 2 /
M U N G U R O H O M T A K A T I F U
Mila (muendelezo)
Francis, au Dominic, na miongoni mwa Waprotestanti watu kama Martin Luther, John Calvin, Ulrich Zwingli, na John Wesley . Wanawake pia wameanzisha harakati muhimu za imani ya Kikristo (mfano, Aimee Semple Mcpherson wa Kanisa la Foursquare ), pamoja na wale wenye mikusanyiko midogo kidogo (mfano, Richard Allen wa Kanisa la The African Methodist Episcopal Church au Charles H. Mason wa The Church Of God In Christ , ambaye pia alisaidia kukua kwa Kanisa la Assemblies Of God ). Wote hawa walijaribu kuonyesha Mapokeo Yenye Mamlaka na Mapokeo Makuu katika njia fulani mahususi inayoendana na wakati wao na namna yao ya utendaji kazi. Kutokea kwa harakati za Imani zenye tija na matokeo makubwa katika nyakati tofauti na kwa watu tofauti kunafunua utendaji wa Roho Mtakatifu kwa wakati wote katika historia. Hivyo ndani ya Ukatoliki, jumuiya mpya zimetokea, kama vile Wabenedikti, Wafransisko, na Wadominika, na nje ya Ukatoliki, madhehebu mapya yametokea kama vile (Walutheri, Wapresbiteri, Wamethodisti, Kanisa la Mungu katika Kristo n.k.). Kila moja ya mapokeo haya haya ina “waanzilishi,” Viongozi wakuu ambao nguvu na maono yao vilisaidia kuanzisha aina ya kipekee ya imani ya kikristo na utendaji wake. Bila shaka, ili ziwe halali, harakati hizi, lazima zilenge na kuelezea kwa uaminifu Mapokeo Yenye Mamlaka na Mapokeo Makuu. Washirika wa Mila hizi husika wanashikilia mapokeo yao wenyewe na mfumo wa kiroho, lakini mambo haya sio lazima yawe mambo ya lazima kwa Kanisa kwa ujumla. Bali yanawakilisha namna ya kipekee ya ufahamu wa jumuiya husika, na uaminifu wao kwenye Mapokeo Yenye Mamlaka na Mapokeo Makuu. Mapeleo mahususi hutafuta kuonyesha na kuuishi uaminifu huu kwa Mapokeo Yenye Mamlaka na Mapokeo Makuu kupitia ibada, mafundisho na huduma zao. Wanatafuta kufanya injili ieleweke katika tamaduni mpya mpaka zile zilizo katika jamii ndogo kabisa, zikiongelea na kutengeneza tumaini la Kristo katika hali mpya ambazo zimetengenezwa na namna ya utaratibu walionayo kulingana na masuala yao wenyewe. Hivyo harakati hizi zinalenga kuonyesha muktadha halisi wa Mapokeo Makuu kwa namna ambayo kwa ubora na ufasaha zinaongoza makundi mapya ya watu katika imani ya Kristo, na zinawashirikisha wale ambao wana amini katika jumuiya ya imani inayotii mafundisho yake na kusema ushuhuda wake kwa wengine.
Made with FlippingBook Digital Proposal Maker