Mungu Roho Mtakatifu, Kitabu cha Mwanafunzi, Capstone Module 14 Swahili Student Workbook
/ 1 7 9
M U N G U R O H O M T A K A T I F U
K I A M B A T I S H O C H A 1 6 Mifano ya Matamko ya Kimadhahebu kuhusu “Ubatizo katika Roho Mtakatifu” Ambayo Yanaelezea Mitazamo Tofauti Kanisa la Kiinjili la Presbitaria Imetolewa kutoka katika Tamko la Msimamo kuhusu Roho Mtakatifu, www.epc.org/about-epc/position-pa pers/holy-spirit.html Kama dhehebu katika mapokeo ya Matengenezo [Reformed] , tunakubali uthibitisho wa kale wa imani ya Kikristo ya kiothodoksi na tunaamini katika “Bwana mmoja, imani moja, ubatizo mmoja” (Waefeso 4:5). Ubatizo huu, ambao unaonyeshwa wazi katika sakramenti ya agano inayobeba jina lake, ni kazi isiyoonekana ya Roho ambayo hufanyika wakati wa kuzaliwa upya. Paulo anaeleza ukweli huu katika 1 Wakorintho 12:13, anapowaambia Wakorintho “…sisi sote tulibatizwa katika Roho mmoja katika mwili mmoja…” Kwa hivyo, tunashikilia dhana ya ubatizo katika au kwa Roho Mtakatifu kama tendo la Roho ambalo humchukua mtu ambaye hajazaliwa upya na, kupitia kuzaliwa upya, humfanya kuwa mwana katika familia ya Mungu. Kazi zote za Roho zinazofuata, basi, ni kwa sababu ya ubatizo huu wa awali na si kwamba zimejitenga nao. Kwa kuwa Wakristo wameitwa “…kujazwa na Roho…” (Waefeso 5:18) waamini wote katika Kristo, wakiwa wamebatizwa katika mwili wake kwa Roho Mtakatifu, wanapaswa kutafuta kuona utimilifu wa amri hii. Tunaamini kwamba Wakristo wameitwa kutangaza neema inayotolewa ili kusamehe, kukomboa na kutoa nguvu mpya za kiroho katika maisha kupitia Yesu Kristo na ujazo wa Roho Mtakatifu.” (Book of Worship, 1-3). Kanisa la Mnazareti Imetolewa kutoka katika Tamko la Imani (Article of Faith), www.nazarene.org/gensec/we_believe.html Tunaamini kwamba utakaso kamili ni lile tendo la Mungu, linalofuata baada ya kuzaliwa upya, ambalo kwa hilo waamini wanawekwa huru na dhambi ya asili, au upotovu, na kuletwa katika hali ya kujitoa kwa Mungu kikamilifu, na kwa utakaso huo utii mtakatifu wa upendo hukamilishwa. Unafanyika kwa njia ya ubatizo wa Roho Mtakatifu, na unahusisha, katika tendo moja, utakaso wa moyo dhidi ya dhambi na uwepo wa kudumu wa Roho Mtakatifu, kwa kukaa kwake ndani ya mwamini, akimwezesha kwa ajili ya maisha na huduma.
Mtazamo wa Ubatizo wa Roho kama Tendo la Mara Moja
Ubatizo wa Roho Kama Tendo Lenye Hatua Nyingi: Mtazamo wa Makanisa ya Holiness
Made with FlippingBook Digital Proposal Maker