Mungu Roho Mtakatifu, Kitabu cha Mwanafunzi, Capstone Module 14 Swahili Student Workbook

1 8 0 /

M U N G U R O H O M T A K A T I F U

Mifano ya Matamko ya Kimadhahebu kuhusu “Ubatizo katika Roho Mtakatifu” (muendelezo)

Utakaso kamili hutolewa kwa damu ya Yesu, unafanywa mara moja kwa imani, hutanguliwa na kujiweka wakfu kikamilifu; na Roho Mtakatifu hushuhudia juu ya kazi na hali hii ya neema. Uzoefu huu pia unajulikana kwa maneno mbalimbali yanayowakilisha awamu zake tofauti, kama vile “ukamilifu wa Kikristo,” “upendo mkamilifu,” “usafi wa moyo,” “ubatizo wa Roho Mtakatifu,” “utimilifu wa baraka,” na “Utakatifu wa Kikristo.” Tunaamini kwamba kuna tofauti kubwa kati ya moyo safi na ukomavu wa tabia. Ya kwanza hupatikana mara moja, kama matokeo ya utakaso kamili; ya pili ni matokeo ya kukua katika neema. Tunaamini kwamba neema ya utakaso kamili inajumuisha msukumo wa kukua katika neema. Hata hivyo, msukumo huu lazima uendelezwe kwa uangalifu, na uangalizi wa karibu utolewe kwa mahitaji na mchakato wa ukuaji wa kiroho na kule kufanywa kuwa bora katika kumfanania Kristo katika tabia na utu. Pasipo jitihada za makusudi kama hizo ushuhuda wa mtu unaweza kuharibika na neema yenyewe ikazongwa na hatimaye kupotea. Kanisa la Assemblies of God Imetolewa kutoka katika Ushahidi wa Nje wa Kimwili wa Ubatizo katika Roho Mtakatifu (The Initial Physical Evidence of Baptism in the Holy Spirit), http://ag.org/top/position_papers/0000_index.cfm Neno ubatizo katika Roho Mtakatifu limechukuliwa kutoka katika Maandiko. Yohana Mbatizaji alikuwa wa kwanza kulitumia muda mfupi kabla ya Yesu kuanza huduma Yake ya hadharani. Alisema, “Yeye [Yesu] atawabatiza kwa Roho Mtakatifu” (Mathayo 3:11). Mwishoni mwa huduma Yake duniani, Yesu alirejelea maneno ya Yohana (Matendo 1:5); na Petro, katika kuripoti matukio katika nyumba ya Kornelio, pia alirudia kauli hiyo (Matendo 11:16). Ubatizo katika Roho (unaorejelewa pia humu kama Ubatizo) hutokea baadaye na ni tofauti na kuzaliwa upya. Maandiko yanaweka wazi kuwa kuna tukio ambalo Roho Mtakatifu huwabatiza waamini katika mwili wa Kristo (1 Wakorintho 12:13), na kuna tukio ambalo Kristo huwabatiza waamini katika RohoMtakatifu (Mathayo 3:11). Haya hayawezi kumaanisha tukio lile lile kwa kuwa wakala anayebatiza na jambo ambalo muhusika anabatizwa kwalo ni tofauti katika kila tukio. Utofauti wamatukio hayo unaonyeshwa katika sehemu kadhaa. Kisa cha wanafunzi wa Efeso ni mfano mmojawapo. Baada ya kusema kwamba walikuwa wamepokea ubatizo wa Yohana pekee (Matendo 19:3), Paulo aliwaeleza kwamba walipaswa

Ubatizo wa Roho Kama Tendo Lenye Hatua Nyingi: Mtazamo wa Makanisa ya Kipentekoste

Made with FlippingBook Digital Proposal Maker