Mungu Roho Mtakatifu, Kitabu cha Mwanafunzi, Capstone Module 14 Swahili Student Workbook
/ 1 9 3
M U N G U R O H O M T A K A T I F U
Maeneo Ambayo Wakristo Wanatofautiana Kuhusiana na Karama za Rohoni (muendelezo)
wa Neno hilo, likilinda amana ya imani lakini sio kuiongeza au kuipunguza. 1) Yuda 1:3 – Wapenzi, ijapokuwa nilitaka sana kuwaandikia juu ya wokovu ambao ni wetu sisi sote, naliona imenilazimu kuwaandikia ili niwaonye kwamba mwishindanie imani waliyokabidhiwa watakatifu mara moja tu. (2) Waebrania 1:1-3 –Mungu, ambaye alisema zamani na baba zetu katika manabii kwa sehemu nyingi na kwa njia nyingi, 2 mwisho wa siku hizi amesema na sisi katika Mwana, aliyemweka kuwa mrithi wa yote, tena kwa yeye aliufanya ulimwengu. 3 Yeye kwa kuwa ni mng’ao wa utukufu wa Mungu na chapa kamili ya nafsi yake, akivichukua vyote kwa amri ya uweza wake, akiisha kufanya utakaso wa dhambi, aliketi katika mkono wa kulia wa Ukuu huko juu; (3) Wagalatia 1:8-9 – Lakini hata ikiwa sisi au malaika kutoka mbinguni atawahubiri ninyi injili tofauti na ile tuliyowahubiri, na alaaniwe. 9 Kama tulivyotangulia kusema, na sasa nasema tena, Mtu awaye yote akiwahubiri ninyi injili kinyume na ile mliyoipokea, na alaaniwe. B. Baadhi ya mapokeo (imani za madhehebu) hujibu “Ndiyo.” “Wote wanaweza kukubaliana kwamba hakuna ufunuo mpya unaoweza kutarajiwa kuhusu Mungu katika Kristo. Lakini inaonekana hakuna sababu nzuri kwa nini Mungu aliye hai, ambaye hunena na kutenda (tofauti na sanamu zilizokufa), hawezi kutumia karama ya unabii kutoa mwongozo kwa kanisa la mahali fulani, taifa au mtu binafsi, au kuonya au kutia moyo kwa njia ya kutabiri na kwa maonyo, sawasawa na neno lililoandikwa la Maandiko Matakatifu, ambalo kwa hilo maneno hayo yote lazima yajaribiwe. Ni kweli, Agano Jipya halionyeshi kuwa kazi ya nabii ni kuwa mvumbuzi wa mafundisho, bali kutoa neno ambalo Roho humpa kulingana na kweli waliokabidhiwa mara moja watakatifu (Yuda 3), kuchochea na kutia moyo imani yetu.” (J. P. Baker, “Prophecy,” New Bible Dictionary, 2 nd Edition, J. D. Douglas and Others, eds).
Made with FlippingBook Digital Proposal Maker