Mungu Roho Mtakatifu, Kitabu cha Mwanafunzi, Capstone Module 14 Swahili Student Workbook

/ 1 9 7

M U N G U R O H O M T A K A T I F U

Kazi ya Roho Mtakatifu katika Uongozi wa Kiroho (muendelezo)

maamuzi ya hekima ni ishara muhimu ya ukomavu wa kiroho. Na zaidi, ni jambo ambalo tunajifunza tunapoendelea kukomaa katika imani na kukua katika hekima. ~ Gordon T. Smith. The Voice of Jesus: Discernment, Prayer, and the Witness of the Spirit. Kurasa za 130-132.

III. Tunaisikiaje Sauti ya Mungu ?

A. Fahamu kile ambacho Mungu Roho amekwisha kukisema tayari: Neno la Mungu lililoandikwa.

1. Maandiko ni kumbukumbu ya mwongozo wa Roho. Maandiko sio tu kipimo kisicho na makosa cha usahihi wa maelekezo ya kiroho au unabii, yenyewe pia ni mafunzo yetu katika kuitambua sauti ya Mungu.

2. Yohana 5:46-47 –Kama mngalimwamini Musa, mngeniamini Mimi; kwa sababu Yeye aliandika habari zangu 47 Lakini msipoyaamini Maandiko yake, mtayaamini wapi maneno yangu?

B. Elekeza moyo wako kutii

1. Kwa kawaida, tatizo HALIKO katika kusikia kwetu!

a. Zab. 119:10 –Kwa moyo wangu wote nimekutafuta; usiniache nipotee mbali na maagizo yako!

b. Swali la msingi linalohusiana na maongozi ya Roho si kama nitaweza kumsikia Mungu akisema bali kama ninakusudia kutii anachosema.

Made with FlippingBook Digital Proposal Maker