Mungu Roho Mtakatifu, Kitabu cha Mwanafunzi, Capstone Module 14 Swahili Student Workbook
1 9 8 /
M U N G U R O H O M T A K A T I F U
Kazi ya Roho Mtakatifu katika Uongozi wa Kiroho (muendelezo)
2. Mungu ni kiongozi mwenye uwezo, anayezungumza kwa uwazi.
a. Yohana 10:2-5, 27 – Aingiaye mlangoni ni mchungaji wa kondoo. 3 Bawabu humfungulia huyo, na kondoo humsikia sauti yake; naye huwaita kondoo wake kwa majina yao, na kuwapeleka nje. 4 Naye awatoapo nje kondoo wake wote, huwatangulia; na wale kondoo humfuata, kwa maana waijua sauti yake. 5 Mgeni hawatamfuata kabisa, bali watamkimbia; kwa maana hawazijui sauti za wageni…. 27 Kondoo wangu waisikia sauti yangu; nami nawajua, nao wanifuata. b. Mifano yaMaandiko inamwelezeaMungu ambayewatuwatamsikia! (1) Lugha za picha zinazotolewa na Mungu kuelezea uongozi wake zinasaidia sana. Mungu ni mfalme, mzazi, mchungaji. Swali la “Tunasikiaje?” ni hadimu sana katika Biblia. Yesu anasema kwa ujasiri kabisa kwamba kondoo wake wanaijua sauti yake. Kama wafalme au wazazi au wachungaji wote, Mungu hashindwi kuwasiliana nasi kwa njia ambazo tutaelewa. (2) Je, ni wangapi kati yetu, kwa mfano, wameona Shirika la TRA likipata ugumu wa kuwasiliana nasi tukuambia tunapaswa kulipa kodi? Je! ni wangapi kati yetu ambao husahau au hujisahaulisha tu tarehe ya kulipa kodi na wasiifikirie tena mara tu inapokuwa imepita? (3) Ni wangapi kati yetu ambao mkiwa watoto mlijikuta mahala fulani mkiwa na huzuni kubwa kwa sababu hamkuwa na uhakika kama mtaweza kutambua sauti za wazazi wenu. Ulifanya nini ukiwa mtoto mchanga ili kuhakikisha unapata uwezo wa kuwasikia na kuwaelewa wazazi wako? (4) Vivyo hivyo, Mungu huchukua hatua ya kwanza kuwajulisha watu wake mapenzi yake.
c. Mungu anaponyamaza mara nyingi inamaanisha kwamba anatupa uhuru wa kuchagua chochote kati ya machaguo mengi mazuri ambayo ametuwekea, au vinginevyo, Mungu akinyamaza maana
Made with FlippingBook Digital Proposal Maker