Mungu Roho Mtakatifu, Kitabu cha Mwanafunzi, Capstone Module 14 Swahili Student Workbook
/ 1 9 9
M U N G U R O H O M T A K A T I F U
Kazi ya Roho Mtakatifu katika Uongozi wa Kiroho (muendelezo)
yake ni kwamba tunafanya kazi chini ya amri na maelekezo ambayo tayari alikwisha kuyatoa hapo awali [yaani hatuhitaji maelekezo mapya]. (1) Ikiwa Mungu anataka tufanye jambo fulani, atalifanya jambo hilo liwe wazi kwa kila moyo unaosikiliza. (2) Wakati Mungu tayari ametufunulia mapenzi yake kupitia Maandiko, swali halitakuwa tena kwa habari ya tutasikiaje bali ni suala la utii. d. Umuhimu wa moyo unaosikiliza. Kanuni ya msingi: Hatuwezi kuwa tunampuuza Mungu au kukwepa kutii na kisha kudai kwamba Mungu hasemi chochote. (1) Kanisa la Mungu kama mazingira ya asili ya kusikiliza. (a) M fano wa familia ni wa kweli. Watoto wangu walikuja nyumbani baada ya shule kila siku, walikula mezani pangu, waliishi nyumbani kwangu, na kushiriki katika maisha ya familia yetu. Kwa sababu walifanya hivyo, walikuwa na uhakika kwamba walisikia nilichotaka kutoka kwao. Ni lazima tufanye vivyo hivyo katika mwenendo wetu wa kiroho. (b) T ukipuuza uhusiano wetu na familia ya Mungu na tusipotumia muda wetu mbele zake, na kusikia Neno lake, atasema, lakini uwezekano mkubwa ni kwamba hatutasikia sauti yake. Kwa upande mwingine, kushiriki kwa bidii katika maisha ya familia ni sehemu muhimu katika kujenga uwezo wetu wa kusikia na kusikiliza. (c) Katika uzoefu wangu mwenyewe, Mungu mara nyingi
huzungumza nami kanisani. Wakati mwingine kupitia mahubiri na wakati mwingine kupitia kitu kingine tofauti kabisa na mahubiri au msisitizo wa ibada. Jambo la msingi ni kwamba niko kwenye meza ya familia yake. Anaweza kuongea kupitia mhubiri au anaweza tu kunasa usikivu wangu na kuzungumza moja kwa moja na moyo wangu
Made with FlippingBook Digital Proposal Maker