Mungu Roho Mtakatifu, Kitabu cha Mwanafunzi, Capstone Module 14 Swahili Student Workbook

2 0 0 /

M U N G U R O H O M T A K A T I F U

Kazi ya Roho Mtakatifu katika Uongozi wa Kiroho (muendelezo)

lakini lazima nishiriki katika familia ili kuwa na matarajio ya kupokea maongozi yake. Ikiwa tunakimbia mbali na hatuwi na wakati na familia ya Mungu (kama mwana mpotevu) hatuwezi, basi, kuwa na visingizio kwamba hatumsikii akisema chochote. (d)  Kusikia sauti ya Mungu si lazima liwe jambo la faragha. Kunatokea katika jumuiya. Tunasikia sauti ya Mungu vizuri zaidi tunaposikiliza pamoja na wengine. (e)  Wachungaji wetu na viongozi wetu wa kiroho wana nafasi ya kipekee katika mchakato huu. (f)  Ebr. 13:17–Watiini viongozi wenu, na kuwanyenyekea; maana wao wanakesha kwa ajili ya roho zenu, kama watu watakaotoa hesabu, ili kwamba wafanye hivyo kwa furaha wala si kwa huzuni; maana haitawafaa ninyi. (g)  Kuzungumza na viongozi na wachungaji wetu ili kupata maarifa na ushauri wao ni hatua ya asili ya kuanzia katika suala zima la maamuzi pale ambapo mapenzi ya Mungu hayako wazi. (h) N dugu na dada zetu katika Kristo pia ni vyanzo muhimu vya kutujulisha nia ya Kristo kwetu. (i)  1 Kor. 12:7–Lakini kila mmoja hupewa ufunuo wa Roho kwa kufaidiana. (j)  1 Kor. 14:26–Basi, ndugu, imekuwaje? Mkutanapo pamoja, kila mmoja ana zaburi, ana fundisho, ana ufunuo, ana lugha, ana tafsiri. Mambo yote na yatendeke kwa kusudi la kujenga. (k)  Mit. 27:17–Chuma hunoa chuma, ndivyo mtu aunoavyo uso wa rafiki yake. (l)  Mit. 11:14–Pasipo mashauri taifa huanguka; Bali kwa wingi wa washauri huja wokovu. (m)  Kuisikiliza sauti ya Roho ina maana kwamba lazima tusikilize ushauri wa jumuiya ya kanisa na viongozi wake.

Made with FlippingBook Digital Proposal Maker