Mungu Roho Mtakatifu, Kitabu cha Mwanafunzi, Capstone Module 14 Swahili Student Workbook
2 0 4 /
M U N G U R O H O M T A K A T I F U
Baadhi ya Njia Ambazo Wakristo Hawakubaliani kuhusu Utakaso (muendelezo)
b. Warumi 7 – Kifungu hiki kinaeleweka kama kinachoelezea uzoefu wa Paulo baada ya kuoka.
c. Ukamilifu kamili usio na dhambi haupatikani katika maisha haya. Neno “Kamili” linapotokea katika Maandiko linamaanisha “timilifu” au “~a kukomaa.” Kutukuzwa ni kiwango cha kutokuwa na dhambi kabisa . Utakaso ni mwendo na safari ya kuelekea utakatifu unaotumia nyenzo zinazotolewa wakati wa wokovu. d. Mtetezi muhimu zaidi wa kihistoria: Martin Luther Luther alizungumza kuhusu Wakristo kama “simul justus et peccator” – Mtu mwenye haki ambaye pia ni mwenye dhambi. Aliamini kwamba kitendawili hiki hakitapata suluhu hadi imani iwe dhahiri kwa kuonekana. Ulutheri hautetei dhambi hata kidogo. Badala yake unatambua “kwamba dhambi ilipozidi, neema ilizidi zaidi.” A. Utakaso ni tendo la pili ambalo ni tofauti na wokovu. Lakini ni kama tu wokovu unavyopokelewa, utakaso huu pia unapokelewa kwa neema kwa njia ya imani na mara nyingi unaelezewa kama “Ubatizo katika Roho Mtakatifu.” Utakaso kamili ambao unajulikana zaidi kama “utakaso,” “utakatifu,” “ukamilifu wa Kikristo,” au “upendo mkamilifu,” unawakilisha ile hatua ya pili ya uhakika katika maisha wa Kikristo ambapo, kwa ubatizo wa Roho Mtakatifu unaotolewa na Yesu Kristo na kupokelewa papo hapo kwa imani, mwamini aliyehesabiwa haki anakombolewa kutoka katika dhambi ya asili, na kwa sababu hiyo huokolewa kutokana na hasira zote zisizo njema, husafishwa kutokana na unajisi wote wa kimaadili, hukamilishwa katika upendo na kuingizwa katika ushirika kamili na wa kudumu na Mungu. ~ Azimio la Mkutano Mkuu wa Kwanza wa Kanisa la Holiness
III. Vuguvugu la Holiness
Kuhusu Fundisho, uliofanyika Chicago, Mei, 1885 [Robert M. Anderson, Vision of the Disinherited ]
Made with FlippingBook Digital Proposal Maker