Mungu Roho Mtakatifu, Kitabu cha Mwanafunzi, Capstone Module 14 Swahili Student Workbook
/ 2 0 5
M U N G U R O H O M T A K A T I F U
Baadhi ya Njia Ambazo Wakristo Hawakubaliani kuhusu Utakaso (muendelezo)
B. Dhambi kimsingi inafafanuliwa kama “Kukosa utii kwa kujua na kwa makusudi.”
1. Dhana ya Ukamilifu wa Kikristo [utakaso kamili] imefafanuliwa kwa umakini namna hii. Ukamilifu sio: maarifa kamili (ujinga unabaki), sio uhuru kutokana na makosa, sio uhuru kutokana udhaifu au kasoro za kitabia, sio uhuru kutokana na majaribu, sio uhuru kutokana na hitaji la kukua, [Mtazame John Wesley, katika kitabu chake kuhusu Ukamilifu wa Kikristo, On Christian Perfection]. Siyo, kupoteza uwezo wa kutenda dhambi. Hakuna hatua ambapo, kabla ya Kutukuzwa, watu walikosa kuanguka. Ukamilifu ni: Kutembea katika upendo kwa imani ili mtu asitende dhambi kwa makusudi na kimazoea. 2. Bado kuna mchakato wa utakaso unaofuata baada ya tukio la utakaso. Ninaamini ukamilifu huu daima unafanyika ndani ya roho kwa tendo rahisi la imani; ni tukio linalofuata na la papo hapo. Lakini ninaamini pia [katika] kazi ya endelevu, iliyotangulia na kufuatia tukio hilo. Kwa habari ya muda, naamini tukio hili kwa ujumla ni tukio la kifo, muda kabla ya roho kuondoka katika mwili. Lakini naamini linaweza kuwa miaka kumi, ishirini, au arobaini kabla. Na ninaamini kwa kawaida ni miaka mingi baada ya kuhesabiwa haki. ~ Mawazo kadhaa kwa ufupi kuhusu Ukamilifu wa Kikristo. The Works of John Wesley. Vol. 11, uk. 466. Baadhi ya makundi ya Holiness hayakubaliani na Wesley kuhusiana na upangiliaji wa muda kama alivyoonyesha yeye. Wanaamini utakaso kamili unaweza, na unapaswa, kuja haraka zaidi.
Made with FlippingBook Digital Proposal Maker