Mungu Roho Mtakatifu, Kitabu cha Mwanafunzi, Capstone Module 14 Swahili Student Workbook
2 0 6 /
M U N G U R O H O M T A K A T I F U
Baadhi ya Njia Ambazo Wakristo Hawakubaliani kuhusu Utakaso (muendelezo)
C. Hoja zinazokubaliana na msimamo huu:
1. Utakatifu Kamili umeamrishwa na Yesu na Mitume Mt. 5:48 “Basi ninyi iweni wakamilifu, kama Baba yenu wa mbinguni alivyo mkamilifu.” Linganisha na agizo la Mtume (1 Yohana 5:3 - Kwa maana huku ndiko kumpenda Mungu: kwamba tuzishike amri zake. Wala amri zake si nzito).
2. Ni maana ya kimantiki ya kile kinachotokea wakati Mungu mwenye uweza wote anapomweka Roho wake kufanya kazi dhidi ya dhambi katika maisha yetu.
3. Maandiko yanaonekana kumaanisha mara kwa mara kwamba hicho ndicho kinachotokea katika maisha ya mwamini.
4. Warumi 7 – Kifungu hiki kinaaminika kuwa kinaelezea uzoefu wa Paulo kabla ya kuokoka.
D. Mtetezi muhimu zaidi wa kihistoria wa dhana hii: John Wesley (aliyejifunza kutoka kwa mwandishi wa kipuritani, William Law)
E. Chanzo Muhimu: Kitabu cha “Maelezo ya wazi ya Ukamilifu wa Kikristo” (“A plain Account of Christian Perfection”) Hoja kuu ya Wesley ilikuwa ni kuepuka kukana uwezekano wa ukamilifu kwa sababu alihisi kuwa inapinga asili na nguvu za Mungu. (Usiseme kwamba Mungu hawezi au hatafanya kile ambacho ni kwamba dhahiri anataka kufanya). Ni suala la imani kwa Wesley. Hata kama hajawahi kuona hili likitokea bado aliamini katika uwezo wa Mungu wa kutimiza shauku yake ya utakatifu wetu.
Made with FlippingBook Digital Proposal Maker