Mungu Roho Mtakatifu, Kitabu cha Mwanafunzi, Capstone Module 14 Swahili Student Workbook
/ 2 0 7
M U N G U R O H O M T A K A T I F U
Baadhi ya Njia Ambazo Wakristo Hawakubaliani kuhusu Utakaso (muendelezo)
IV. Kuweka vyote Pamoja: Msingi wa Pamoja wa Kitheolojia na Maana zake Muhimu Yale ambayo Wakristo wa Makanisa ya Matengenezo yaani Reformed na Holiness wanakubaliana kwa pamoja: A. Utakaso ni kuwa kama Kristo na ndio lengo la maisha ya Kikristo. [Maandiko yanatufundisha kwamba [utakatifu] huu ndilo lengo la wito wetu – John Calvin, katika kitabu chake cha “Institutes of the Christian Religion ].
B. Utakaso huanza wakati wa wokovu na sharti pekee linalohitajika ni imani. Tazama (Nyaraka za Fundisho za Mitaguso ya Wamethodisti za mwaka 1744-47).
C. Utakaso huja kwa kuhesabiwa na kupewa kama kipawa na huja kwa neema ya Mungu tu.
D. Utakaso unahusisha hatua ya kipekee ya uamuzi 1 namchakato unaoendelea wa kuishi kutokana na uamuzi huo.
1 Kwa Theolojia ya Makanisa ya Reformed hatua hii ni ile ya kuupokea wokovu, kwa Theolojia ya Makanisa ya Holiness hatua hii ni kuupokea wokovu na tukio la pili la neema la Roho Mtakatifu
Made with FlippingBook Digital Proposal Maker