Mungu Roho Mtakatifu, Kitabu cha Mwanafunzi, Capstone Module 14 Swahili Student Workbook
2 0 8 /
M U N G U R O H O M T A K A T I F U
K I A M B A T I S H O C H A 2 2 Misimamo ya Madhehebu Mbali-mbali Kuhusu “Utakaso”
Kanisa la Ndugu wa Kilutheri http://www.clba.org/aboutus.phtml Utakaso
Makala kutoka Madhehebu ya Kilutheri, Reformed, na ya Kibaptisti
Utakaso ni kazi ya neema ya Mungu, kazi endelevu ya kufanywa upya kiroho na ya ukuaji katika maisha ya kila mtu aliyehesabiwa haki. Kwa njia ya neema, Roho Mtakatifu anafanya kazi ya kuzaa tabia ya Kristo ndani ya maisha ya waamini wote, akiwafundisha na kuwahimiza kuiishi asili yao mpya. Roho Mtakatifu huwawezesha waamini zaidi na zaidi kumpinga shetani, kuushinda ulimwengu, na kujihesabu kuwa wafu kwa dhambi lakini walio hai kwa Mungu katika Kristo Yesu. Roho Mtakatifu huzaa tunda la roho na kuwapa karama za rohoni waamini wote. Anawaita, anawaimarisha na kuwawezesha kumtumikia Mungu nyumbani, katika jamii na kama sehemu ya Kanisa la Ulimwengu. Mchakato wa utakaso utakamilika pale tu mwamini atakapofikia utukufu.
Kanisa la Wapresibiteri la Marekani http://www.pcanet.org/general/cof_chapxi-xv.htm#chapxiii
Tamko la Imani la Westminster SURA YA. XIII. -Ya Utakaso.
1. H ao ambao wakati fulani waliitwa kikamilifu, na kuzaliwa upya, wakiwa na moyo mpya, na roho mpya iliyoumbwa ndani yao, wanazidi kutakaswa, kihalisia na kibinafsi, kwa nguvu ya kifo na ufufuo wa Kristo, kwa Neno lake na Roho wake anayekaa ndani yao, nguvu ya mwili wote wa dhambi yanaharibiwa, na tamaa zake zinazidi kudhoofika na kufishwa; nao wanazidi kuhuishwa na kuimarishwa katika neema zote za wokovu, kwa kuuishi utakatifu wa kweli, ambao hapana mtu atakayemwona Bwana asipokuwa nao. 2. U takaso huu ni kamili, ndani ya kila sehemu ya mtu; lakini bado haujakamilika katika maisha haya, katika kila sehemu yamebaki baadhi ya mabaki ya uharibifu; ambapo hutokea vita vya mara kwa mara na visivyoweza kusuluhishwa, mwili ukitamani kinyume cha matamanio ya Roho, na Roho kinyume cha mwili. 3. K atika vita hiyo, ingawa uharibifu uliobaki, kwa muda, unaweza kutawala sana; walakini, kupitia nguvu ambazo Roho Mtakatifu wa Kristo anaendelea
Made with FlippingBook Digital Proposal Maker