Mungu Roho Mtakatifu, Kitabu cha Mwanafunzi, Capstone Module 14 Swahili Student Workbook
/ 2 0 9
M U N G U R O H O M T A K A T I F U
Matamko ya Kidhehebu Kuhusiana na “Utakaso” (muendelezo)
kuzitoa, sehemu iliyozaliwa upya inashinda; na hivyo, watakatifu wanakua katika neema, wakiukamilisha utakatifu katika kumcha Mungu.
Mkutano wa Wabaptisti wa Kusini http://www.sbc.net/bfm/bfm2000.asp#iv
Wokovu unahusisha ukombozi wa mwanadamu mzima, na hutolewa bure kwa wote wanaomkubali Yesu Kristo kuwa Bwana na Mwokozi, ambaye kwa damu yake mwenyewe aliupata ukombozi wa milele kwa ajili ya mwamini. Katika maana yake pana, wokovu unajumuisha kuzaliwa upya, kuhesabiwa haki, utakaso, na kutukuzwa. Hakuna wokovu isipokuwa kwa njia ya imani ya binafsi katika Yesu Kristo kama Bwana. 1. K uzaliwa mara ya pili, au kuzaliwa upya, ni kazi ya neema ya Mungu ambapo waamini wanakuwa viumbe vipya katika Kristo Yesu. Ni badiliko la moyo linalofanywa na Roho Mtakatifu kwa njia ya kuhakikisha kwa habari ya dhambi, ambapo mwenye dhambi huitikia kwa toba kwa Mungu na imani katika Bwana Yesu Kristo. Toba na imani ni vipengele vya neema visivyoweza kutenganishwa. T oba ni kugeuka kwa kweli kutoka katika dhambi kuelekea kwa Mungu. Imani ni kumkubali Yesu Kristo na kujitoa mzima-mzima kwake kama Bwana na Mwokozi. 2. K uhesabiwa haki ni tendo la kuachiliwa na kuwa huru kikamilifu kwa neema ya Mungu, kwa msingi wa kanuni za haki yake kwa wenye dhambi wote wanaotubu na kumwamini Kristo. Kuhesabiwa haki humleta mwamini katika uhusiano wa amani na kibali na Mungu. 3. U takaso ni mchakato unaoanza na tendo la kuzaliwa upya, ambapo mwamini anatengwa kimaalum kwa ajili ya Mungu, na kuwezeshwa kusonga mbele kuelekea ukomavu wa kimaadili na kiroho kupitia uwepo na nguvu za Roho Mtakatifu anayekaa ndani yake. Ukuaji katika neema unapaswa kuendelea katika maisha yote ya mtu aliyezaliwa upya. 4. K utukuzwa ni kilele cha wokovu na ni hali ya mwisho ya baraka na ya kudumu ya waliokombolewa. M wa. 3:15; Kut. 3:14-17; 6:2-8; Mt. 1:21; 4:17; 16:21-26; 27:22-28:6; Luka 1:68-69; 2:28-32; Yohana 1:11-14,29; 3:3-21,36; 5:24; 10:9,28-29; 15:1-16;
Made with FlippingBook Digital Proposal Maker