Mungu Roho Mtakatifu, Kitabu cha Mwanafunzi, Capstone Module 14 Swahili Student Workbook
2 1 0 /
M U N G U R O H O M T A K A T I F U
Matamko ya Kidhehebu Kuhusiana na “Utakaso” (muendelezo)
17:17; Mdo 2:21; 4:12; 15:11; 16:30-31; 17:30-31; 20:32; Rum. 1:16-18; 2:4; 3:23-25; 4:3 na kuendelea; 5:8-10; 6:1-23; 8:1-18,29-39; 10:9-10,13; 13:11-14; 1 Kor. 1:18,30; 6:19-20; 15:10; 2 Kor. 5:17-20; Gal. 2:20; 3:13; 5:22-25; 6:15; Efe. 1:7; 2:8-22; 4:11-16; Fil. 2:12-13; Kol. 1:9-22; 3:1 na kuendelea; 1 The. 5:23-24; 2 Tim. 1:12; Tito 2:11-14; Ebr. 2:1-3; 5:8-9; 9:24-28; 11:1-12:8,14; Yakobo 2:14-26; 1 Pet. 1:2-23; 1 Yohana 1:6-2:11; Ufu. 3:20; 21:1-22:5.
Kanisa la Mnazareti www.nazarene.org/gensec/we_believe.html Misingi ya Imani
Makala kutoka kwa Madhehebu ya Holiness
Tunaamini kwamba utakaso kamili ni lile tendo la Mungu, linalofuata baada ya kuzaliwa upya, ambalo kwa hilo waamini wanawekwa huru na dhambi ya asili, au upotovu, na kuletwa katika hali ya kujitoa kwa Mungu kikamilifu, na kwa utakaso huo utii mtakatifu wa upendo hukamilishwa. Unafanyika kwa njia ya ubatizo wa Roho Mtakatifu, na unahusisha, katika tendo moja, utakaso wa moyo dhidi ya dhambi na uwepo wa kudumu wa Roho Mtakatifu, kwa kukaa kwake ndani ya mwamini, akimwezesha kwa ajili ya maisha na huduma. Utakaso kamili hutolewa kwa damu ya Yesu, unafanywa mara moja kwa imani, hutanguliwa na kujiweka wakfu kikamilifu; na Roho Mtakatifu hushuhudia juu ya kazi na hali hii ya neema. Uzoefu huu pia unajulikana kwa maneno mbalimbali yanayowakilisha awamu zake tofauti, kama vile “ukamilifu wa Kikristo,” “upendo mkamilifu,” “usafi wa moyo,” “ubatizo wa Roho Mtakatifu,” “utimilifu wa baraka,” na “Utakatifu wa Kikristo.” Tunaamini kwamba kuna tofauti kubwa kati ya moyo safi na ukomavu wa tabia. Ya kwanza hupatikana mara moja, kama matokeo ya utakaso kamili; ya pili ni matokeo ya kukua katika neema. Tunaamini kwamba neema ya utakaso kamili inajumuisha msukumo wa kukua katika neema. Hata hivyo, msukumo huu lazima uendelezwe kwa uangalifu, na uangalizi wa karibu utolewe kwa mahitaji na mchakato wa ukuaji wa kiroho na kule kufanywa kuwa bora katika kumfanania Kristo katika tabia na utu. Pasipo jitihada za makusudi kama hizo ushuhuda wa mtu unaweza kuharibika na neema yenyewe ikakazongwa na hatimaye kupotea. (Yer. 31:31-34; Eze. 36:25-27; Mal. 3:2-3; Mt. 3:11-12; Luka 3:16-17; Yohana 7:37 39; 14:15-23; 17:6-20; Mdo 1:5; 2:1-4; 15:8-9; Rum. 6:11-13, 19; 8:1-4, 8-14; 12:1 2; 2 Kor. 6:14-7:1; Gal. 2:20; 5:16-25; Efe. 3:14-21; 5:17-18, 25-27; Fil. 3:10-15; Kol. 3:1-17; 1 The. 5:23-24; Ebr. 4:9-11; 10:10-17; 12:1-2; 13:12; 1 Yohana 1:7, 9) (“Ukamilifu wa Kikristo,” “Upendo kamili”: Kum. 30:6; Mt. 5:43-48; 22:37
Made with FlippingBook Digital Proposal Maker