Mungu Roho Mtakatifu, Kitabu cha Mwanafunzi, Capstone Module 14 Swahili Student Workbook

/ 2 1 1

M U N G U R O H O M T A K A T I F U

Matamko ya Kidhehebu Kuhusiana na “Utakaso” (muendelezo)

40; Rum. 12:9-21; 13:8-10; 1 Kor. 13; Fil. 3:10-15; Ebr. 6:1; 1 Yohana 4:17-18 “Usafi wa Moyo”: Mt. 5:8; Mdo 15:8-9; 1 Pet. 1:22; 1 Yohana 3:3 “Ubatizo wa Roho Mtakatifu”: Yer. 31:31-34; Eze. 36:25-27; Mal. 3:2-3; Mt. 3:11-12; Luka 3:16-17; Mdo 1:5; 2:1-4; 15:8-9 “Utimilifu wa baraka”: Rum. 15:29 “Utakatifu wa Kikristo”: Mt. 5:1-7:29; Yohana 15:1-11; Rum. 12:1-15:3; 2 Kor. 7:1; Efe. 4:17 5:20; Fil. 1:9-11; 3:12-15; Kol. 2:20-3:17; 1 The. 3:13; 4:7-8; 5:23; 2 Tim. 2:19-22; Ebr. 10:19-25; 12:14; 13:20-21; 1 Pet. 1:15-16; 2 Pet. 1:1-11; 3:18; Yuda 20-21)

Kanisa la Methodisti Huru www.fmc-canada.org/articles.htm Tamko la Imani

Utakaso kamili ni ile kazi ya Roho Mtakatifu inayofuata baada ya kuzaliwa upya, ambayo kwayo mwamini aliyewekwa wakfu kikamilifu, kwa njia ya imani katika damu ya upatanisho ya Kristo, anasafishwa wakati huo kutoka katika dhambi zote zilizo ndani yake na kutiwa nguvu kwa ajili ya huduma. Uhusiano unaotokea huthibitishwa na ushuhuda wa Roho Mtakatifu na hudumishwa kwa imani na utii. Utakaso kamili humwezesha mwamini kumpenda Mungu kwa moyo wake wote, kwa roho yake yote, kwa nguvu zake zote na kwa akili zake zote, na jirani yake kama nafsi yake, na humtayarisha kwa ukuaji zaidi katika neema. (Law. 20:7 8; Yohana 14:16-17; 17:19; Mdo 1:8; 2:4; 15:8-9; Rum. 5:3-5; 8:12-17; 12:1-2; 1 Kor 6:11; 12:4-5:2; Gal. 5:22-25; Efe. 4:22-24; 1 Thes. 4:7; 5:23-24; 2 Thes. 2:13; Ebr. 10:14)

Kanisa la Wawesley www.wesleyan.org/doctrine.htm Tamko la Imani

Tunaamini kwamba utakaso ni ile kazi ya Roho Mtakatifu ambayo kwayo mtoto wa Mungu anatengwa na dhambi na kutengwa kwa ajili ya Mungu na kuwezeshwa kumpenda Mungu kwa moyo wote na kutembea katika amri zake zote takatifu bila lawama. Utakaso unaanza wakati wa kuhesabiwa haki na kuzaliwa upya. Kuanzia wakati huo kuna utakaso unaoendelea kadiri mwamini anavyotembea na Mungu na kila siku kukua katika neema na katika utii kamili zaidi kwa Mungu. Mchakato huu unamtayarisha kwa ajili ya tukio la utakaso kamili unaofanywa mara moja wakati waamini wanapojitoa kama dhabihu iliyo hai, takatifu na ya kumpendeza

Made with FlippingBook Digital Proposal Maker