Mungu Roho Mtakatifu, Kitabu cha Mwanafunzi, Capstone Module 14 Swahili Student Workbook

2 1 2 /

M U N G U R O H O M T A K A T I F U

Matamko ya Kidhehebu Kuhusiana na “Utakaso” (muendelezo)

Mungu, kwa njia ya imani katika Yesu Kristo, linalotokea kupitia ubatizo wa Roho Mtakatifu ambaye anausafisha moyo na dhambi yote ya asili. Tukio la utakaso kamili humkamilisha mwamini katika upendo na humpa mtu huyo uwezo kwa ajili ya huduma yenye ufanisi. Hilo linafuatiwa na ukuaji wa maisha yote katika neema na ujuzi wa Bwana na Mwokozi wetu Yesu Kristo. Uhai wa utakatifu unaendelea kwa njia ya imani katika damu takatifu ya Kristo na hujidhihirisha yenyewe kwa njia ya utii wa upendo kwa mapenzi ya Mungu yaliyofunuliwa. Mwa. 17:1; Kum. 30:6; Zab. 130:8; Isa. 6:1-6; Eze. 36:25-29; Mt. 5:8, 48; Luka 1:74-75; 3:16-17; 24:49; Yohana 17:1-26; Mdo 1:4-5, 8; 2:1-4; 15:8-9; 26:18; Rum. 8:3-4; 1 Kor. 1:2; 6:11; 2 Kor. 7:1; Efe. 4:13, 24; 5:25-27; 1 The. 3:10, 12-13; 4:3, 7-8; 5:23-24; 2 The. 2:13; Tito 2:11-14; Ebr. 10:14; 12:14; 13:12; Yakobo 3:17-18; 4:8; 1 Petro 1:2; 2 Petro 1:4; 1 Yohana 1:7, 9; 3:8-9; 4:17-18; Yuda 24.

Made with FlippingBook Digital Proposal Maker