Mungu Roho Mtakatifu, Kitabu cha Mwanafunzi, Capstone Module 14 Swahili Student Workbook
3 6 /
M U N G U R O H O M T A K A T I F U
c. Matamko ya kinabii (kama yale yaliyotolewa na Yeremia au Ezekieli).
Katika Agano la Kale, Roho ( rûah ) ya Yahwe ni nguvu ya Mungu katika utendaji.... Ni neno linalomaanisha pumzi iliyopulizwa kadhalika upepo unaovuma.... rûah lina uhusiano halisi na wa ajabu pale linapotumika kumaanisha nguvu za Mungu zilizoachiliwa. Linatumika hivyo karibu mara 100 kati ya mara 400 ambapo
III. Nguvu Itoayo Uzima
A. Roho anahusika kwa karibu sana katika uumbaji wa ulimwengu. Mwanzo 1:1-2 – Hapo mwanzo Mungu aliziumba mbingu na nchi. Nayo nchi ilikuwa ukiwa, tena utupu, na giza lilikuwa juu ya uso wa vilindi vya maji; Roho ya Mungu ikatulia juu ya uso wa maji.
1
1. Roho “ikatulia.”
linatokea katika Agano la Kale. ~“Holy Spirit.”
a. Neno la kiebrania lililotafsiriwa kama “kutulia” ni ( rachaph ) likimaanisha kuchunga kwa umakini (au kuatamia akiwa [hewani] juu ya… linagnisha na Kumb. 32:11). Roho wa Mungu alichunga uumbaji mpya akiuandaa kutoka katika hali ya ukiwa kuwa katika hali yenye mpangilio, toka hali ya giza kuwa nuru. Mwanzo 1:2 - “ pamoja na upepo wa kiungu” b. Kazi ya Roho katika uumbaji wa kimwili inafanana na kazi ya Roho katika “uumbaji mpya” (wokovu) (tazama, Yohana 3). Yohana 3:8 - Upepo huvuma upendako, na sauti yake waisikia, lakini hujui unakotoka wala unakokwenda; kadhalika na hali yake kila mtu aliyezaliwa kwa Roho.
New Dictionary of Theology . Downers Grove, IL/Leicester, England: Inter-Varsity Press, 1988. uk. 316.
Tazama Ray Pritchard, Names of the Holy Spirit . Chicago: Moody Press, 1995. Ukurasa wa 11, 13, 34.
2. Roho ni pumzi ya Mungu ambayo inawaleta wanadamu katika uzima.
a. Mwanadamu wa kwanza, Mwa. 2:7
b. Wanadamu wote, Ayu 33:4, 6
Made with FlippingBook Digital Proposal Maker