Mungu Roho Mtakatifu, Kitabu cha Mwanafunzi, Capstone Module 14 Swahili Student Workbook

/ 3 7

M U N G U R O H O M T A K A T I F U

B. Roho anahusika kwa karibu katika kutegemeza uzima katika ulimwengu.

1. Fundisho la Upaji wa Kiungu.

a. Ufafanuzi: Neno “upaji” [katika mantiki ya utunzaji, providence ] linatokana na neno kutoa. Kwa njia ya upaji wake Mungu anategemeza, anatawala, na kulinda uzima alioutoa katika dunia na kuuongoza hadi mwisho ambao kwa ajili yake uliumbwa.

1

Maana ya msingi ya upaji [utunzaji] ni kuona mbele, au kutoa. Suala la upaji [utunzaji] linahusu jinsi Mungu anavyofikiria mbele zaidi katika kutunza viumbe vyote. . . . Upaji wa Mungu hutazama mbele na kubaini mahitaji ambayo bado hayajatambuliwa na viumbe. Lakini zaidi ya kuona mbele tu, upaji unahusiana na uhifadhi wa kila siku wa Mungu kwa ulimwengu katika hatari zake. ~ Thomas C. Oden. The Living God . uk. 271. b. Kazi ya Roho Mtakatifu katika upaji [utunzaji]: Mpaji wa uzima. (1) Roho yupo kazini kuumba, kufanya upya na kutoa kwa ajili ya aina zote za uzima zilizopo katika uumbaji wake. (2) AK: Zab. 104:29-30; Isa. 32:14-15 (3) AJ: Yoh. 6:63; Rum. 8:2, 6, 11

Kotekote katika ulimwengu, nguvu kubwa sana zinazofanya kazi katika jua, nyota, na makundi ya nyota hutiwa nguvu na Roho wa Mungu. Nishati na nguvu zote zipo kwa uweza wa Roho Mtakatifu. ~ J. Rodman Williams

2. Alama za Roho Mtakatifu katika Biblia zinamfunua yeye kama Mpaji wa uzima.

a. Maji – chanzo cha Uzima. (1) Isaya 44:2-4a

Made with FlippingBook Digital Proposal Maker