Mungu Roho Mtakatifu, Kitabu cha Mwanafunzi, Capstone Module 14 Swahili Student Workbook
4 2 /
M U N G U R O H O M T A K A T I F U
Maswali yafuatayo yaliandaliwa ili kukusaidia kupitia yaliyomo katika sehemu ya pili ya video. Yanalenga utambulisho wa Roho kama mpaji wa uzima. Jibu kwa uwazi na kwa ufupi iwezekanavyo, na tumia Maandiko kujenga hoja zako. 1. Elezea namna ambavyo mawazo ya Agano la Kale na ya Agano Jipya kuhusu Roho wa Mungu yanafanana na namna ambavyo yanatofautiana. 2. Jukumu la Roho katika uumbaji ni lipi? Hili linaonyesha nini kuhusiana na jukumu lake katika wokovu wa waamini (uumbaji mpya)? 3. Upaji [utunzaji] ni nini? Je, Roho ana sehemu gani katika utunzaji wa Mungu kwa ulimwengu? 4. Je, ni ishara gani kuu za Roho Mtakatifu katika Maandiko? Je, haya yanachangiaje katika ufahamu wetu wa Roho kama ndiye atoaye uzima? 5. Je, ni vyeo gani vya kibiblia vya Roho Mtakatifu ambavyo vinasisitiza huduma yake ya kutoa uzima? 6. Ni kwa namna gani huduma ya Roho huleta tumaini kwa waamini wote? Somo hili linahusu Nafsi ya Roho Mtakatifu. Katika mada hii tumejadili kweli zifuatazo: ³ Roho Mtakatifu ni Nafsi ya Tatu ya Mungu Mmoja aliye katika Utatu. ³ Kama alivyo Baba na Mwana, Roho Mtakatifu ni Nafsi ya Kiungu inayo husiana na watu wa Mungu kwa njia binafsi (kuzungumza, kutenda, kuongoza, kufundisha, n.k). ³ Kama vile Yesu alivyokuwa akiwaongoza wanafunzi wake wakati wa huduma yake duniani, Roho Mtakatifu sasa yuko pamoja na Wakristo wote, akiwafundisha, akiwaongoza, na kuwalinda kwa niaba ya Yesu. ³ Roho ametoka kwa Baba na Mwana. Yeye ndiye kielelezo kamili cha upendo wao na ndiye aliyetumwa ulimwenguni kama kipawa cha upendo. ³ Yesu aliwaamuru wafuasi wake kuwabatiza watu wa Mungu katika Jina la Baba, na Mwana, na Roho Mtakatifu. Mitume walihutubia na kuwabariki watu wa Mungu katika Jina la Baba, na Mwana, na Roho Mtakatifu. Viumbe wa mbinguni katika kiti cha enzi cha Mungu humwabudu katika Utatu, wakiita “Mtakatifu, Mtakatifu, Mtakatifu” (Isa. 6:3; Ufu. 4:8).
Sehemu ya 2
Maswali kwa wanafunzi na majibu
1
MUUNGANIKO
Muhtasari wa Dhana Kuu
Made with FlippingBook Digital Proposal Maker