Mungu Roho Mtakatifu, Kitabu cha Mwanafunzi, Capstone Module 14 Swahili Student Workbook
/ 4 3
M U N G U R O H O M T A K A T I F U
Kanisa linafuata nyayo zao, likimuabudu na kumtukuza Mungu kama Baba, Mwana na Roho Mtakatifu. ³ Fundisho la Roho Mtakatifu katika theolojia linajulikana kama neumatologia ( pneumatology) ambalo linatokana na neno la Kiyunani pneuma linalomaanisha roho, pumzi, au upepo. ³ Maandiko yanamfunua Mungu Roho Mtakatifu kama Mpaji wa Uzima ambaye ni muumbaji na mtegemezaji wa maisha yote. ³ Picha na alama zinazotumiwa kumwelezea Roho Mtakatifu katika Biblia zinasisitiza ukweli kwamba Roho Mtakatifu ni Mpaji na Mtegemezaji wa uhai wote. ³ Majina ya kimaandiko ya Roho Mtakatifu yanaonyesha upeo wa huduma yake ya kutoa uzima na hata kumtaja moja kwa moja kama “Roho wa Uzima.” ³ Kusudi la utoaji uzima la Roho Mtakatifu linamaanisha kwamba yeye ndiye chanzo cha tumaini kwa watu binafsi, kwa Kanisa na kwa ulimwengu. Sasa ni wakati wako wa kujadili pamoja na wanafunzi wenzako maswali yako kuhusu mambo ambayo tumejifunza katika somo hili la “Nafsi ya Roho Mtakatifu.” Hata theolojia ya kinadharia zaidi haikusudiwi kuwa “zoezi la kielimu” tu. Kweli za kitheolojia zinakusudiwa kuathiri maisha yetu. Sehemu muhimu zaidi ya kipengele hiki cha maswali na majibu kuhusu Roho Mtakatifu, ni kugundua jinsi Mungu anavyotaka kutubadilisha kupitia yale tuliyojifunza. Je, una maswali gani hasa kwa kuzingatia yale ambayo umejifunza hivi punde? Pengine baadhi ya maswali hapa chini yanaweza kukusaidia kuunda maswali yako mwenyewe, mahususi na ya msingi zaidi. * Mojawapoya tabiazinazofananaza“imani potofu”na ambazozimekuwepo nyakati zote ni kwamba wanafundisha mafundisho yasiyo sahihi kuhusu Mungu. (Iwapo mtu anafundisha upotofu juu ya asili ya Mungu na kweli yake tofauti na jinsi inavyofunuliwa katika Maandiko, hakuna namna anavyoweza kuwakilisha vyema kazi ya Mungu ulimwenguni). Je, ni makosa ya aina gani yanayoweza kutokea kutokana na kufikiria vibaya kuhusu nafsi ya Roho Mtakatifu? * Ufahamu wa ukweli kwamba Roho Mtakatifu ametumwa kama Msaidizi (paracletos), aliyeitwa kuwa pamoja nasi na kuwakilisha uwepo ulio hai wa Yesu katikati yetu, unamatokeo gani kwa mwamini?
1
Kutendea kazi somo na matokeo yake kwa mwanafunzi
Made with FlippingBook Digital Proposal Maker