Mungu Roho Mtakatifu, Kitabu cha Mwanafunzi, Capstone Module 14 Swahili Student Workbook

4 4 /

M U N G U R O H O M T A K A T I F U

* Je, maelezo kuhusu Roho Mtakatifu kama “kifungo cha upendo” kati ya Baba na Mwana yanaathirije uelewa wetu wa jukumu la Roho katika maisha yetu binafsi na makusanyiko ya Kanisa? * Tajabaadhi yanjia zinazofaa ambazomakanisa yetuyanaweza “kumwabudu na kumtukuza Roho” pamoja na Baba na Mwana. * Je, kuna umuhimu wowote katika ukweli kwamba maneno yanayotumika kutafsiri neno “Roho” katika Kiebrania na Kiyunani pia yanamaanisha “pumzi” au “upepo”? Je, dhana hizi zinazohusiana kwa karibu zinatuambia nini kuhusu kazi ya Roho? * Roho Mtakatifu ametendaje kazi kama Mpaji wa Uzima katika maisha yako binafsi? Je, uwezo wake wa kutoa uzima umeleta utofauti gani katika mtazamo wetu juu ya huduma? * Kati ya alama za kimaandiko zinazomwakilisha Roho Mtakatifu, ni zipi zimekuwa muhimu zaidi katika maisha yako binafsi? Je, zimekusaidiaje kumwelewa Roho Mtakatifu? Na zimeathiri vipi uelewa wako wa uongozi wa Kikristo? * Kama Wakristo ambao Roho Mtakatifu anakaa ndani yetu, mara nyingi tunafikiria kazi ya Roho katika mtazamo wa kibinafsi sana: Roho anaishi ndani yangu na kunisaidia kumjua na kumtii Mungu. Je, ni jambo la kawaida kwako pia kumfikiria RohoMtakatifu kama mwenye kuutegemeza uumbaji wote na ambaye anautayarisha ulimwengu kwa ajili ya utawala ujao wa Kristo? (Elezea jibu lako). Unafundisha somo la Roho Mtakatifu katika darasa la Biblia ndani ya kanisa lako na unawakumbusha wanafunzi wako kwamba ni halali kabisa Yeye kuitwa Bwana na Mpaji wa Uzima. Mgeni aitwae Sue, ambaye amekuja kwenye mafundisho mara chache tu, anafurahia anaposikia maelezo yako. Sue anasema, “Kwa kawaida mimi hushiriki ibada katika Kanisa la Unity mtaa wa chini hapo na walinipa kitabu kinachozungumzia jambo hilo hilo.” Anachomoa kitabu na kutafuta kurasa zenye nukuu hizi, “Mungu ni Roho, au kani ya uumbaji ambayo ndiyo chanzo cha vitu vyote vinavyoonekana. . . . Mungu sio kiumbe au nafsi yenye uzima, utashi, upendo na nguvu. . . . Mungu ni yule asiyeonekana, asiyeshikika, lakini ni halisi sana, ni kitu tunachoita uzima. . . . Kila mwamba, mti, mnyama, kila kitu kinachoonekana, ni udhihirisho wa Roho mmoja – Mungu – tofauti ni kiwango tu cha udhihirisho; na kila moja ya njia hizo zisizo na idadi za udhihirisho, au upekee wa kila kimoja, Kuwa Tayari Kutoa Jibu

1

MIFANO

1

Made with FlippingBook Digital Proposal Maker