Mungu Roho Mtakatifu, Kitabu cha Mwanafunzi, Capstone Module 14 Swahili Student Workbook
5 2 /
M U N G U R O H O M T A K A T I F U
Kuitikia Neno la Kinabii
Ibada
Soma 2 Petro 1:16-21 . Mtume Petro alikuwa ameshawishika kabisa kwamba kile alichokiona na kusikia kwenye Mlima wa Mgeuko kilikuwa ni kutumia kwa ushahidi wa kinabii kuhusu Kristo unaopatikana katika Maandiko ya Agano la Kale. Kwa Petro, maneno ya Maandiko ya Kiebrania ni maneno yanayotoka moja kwa moja kwa Roho wa Mungu mwenyewe. Anasema kwamba manabii waliandika Maandiko “wakiongozwa na Roho Mtakatifu.” (Neno lililotafsiriwa “kuongozwa” ni neno lile lile la kiyunani linalotumika katika Matendo ya Mitume 27:17 kuelezea merikebu inayosukumwa mbele na upepo katika matanga yake). Katika ufahamu wa Petro, Roho Mtakatifu aliwabeba manabii kama vile upepo unavyoibeba merikebu. Mwanatheolojia wa kale wa Kikristo, Athenagora, alinasa wazo hilo hilo alipoandika kwamba “... [Manabii] walinena mambo yale yaliyovuviwa. Roho alifanya kazi ndani yao kama vile mpiga filimbi aipulizavyo filimbi.” Kama watu tulioweka imani yetu katika Kristo, tunaamini kwa hakika kwamba Roho Mtakatifu, kwa hakika, alizungumza kupitia manabii. Tunaamini kwamba katika Maandiko tumepata aina ya ukweli ambayo haikutokana na mawazo ya wanadamu bali ilitoka katika fahamu za Mungu mwenyewe. Neno la kiunabii, kama Petro asemavyo, ni “taa inayoangaza mahali penye giza” nasi tunapaswa kulizingatia hilo kikamilifu. Tunaamini kweli kwamba kila nyanja ya elimu ya theolojia tunayojishughulisha nayo inapaswa kuwa jitihada zetu za kuelekeza uzingativu wetu kikamilifu katika Neno la Mungu ambalo limevuviwa na Roho wake. Tunapoanza somo letu, hebu tuanze kwa kumwomba Mungu Roho Mtakatifu aangazie akili zetu si ili tusikie tu, bali pia tuweze kuelewa kikamilifu kweli za neno la kinabii la Mungu. Tunaungana na mtunga Zaburi anapoomba, “Ufumbue macho yangu niyatazame maajabu yatokayo katika sheria yako” (Zab. 119:18). Baada ya kutamka na/au kuimba Kanuni ya Imani ya Nikea (katika Kiambatisho), sali sala ifuatayo: Mungu Mwenyezi, mbele zako mioyo yote iko wazi, kwako haja zote zinajulikana, na kwako hakuna siri iliyofichwa: Safisha mawazo ya mioyo yetu kwa uvuvio wa Roho wako Mtakatifu, ili tuweze kukupenda wewe kikamilifu, na kulitukuza ipasavyo Jina lako takatifu; kwa njia ya Kristo Bwana wetu. Amina. ~ The Book of Common Prayer . New York, NY: The Church Hymnal Corporation, 1979. uk. 355.
2
Kanuni ya Imani ya Nikea na Sala
Made with FlippingBook Digital Proposal Maker