Mungu Roho Mtakatifu, Kitabu cha Mwanafunzi, Capstone Module 14 Swahili Student Workbook

/ 5 3

M U N G U R O H O M T A K A T I F U

Weka kando daftari lako na nyenzo za kujifunzia, kusanya pamoja mawazo yako na tafakuri zako, kisha ufanye Jaribio la Somo la 1, Nafsi ya Roho Mtakatifu .

Jaribio

Mazoezi ya Kukariri Maandiko

Fanya mazoezi pamoja na mwanafunzi mwenzako, andika na/au nukuu kwa kutamka andiko la kukumbuka kutoka kwenye andiko la kipindi kilichopita: Warumi 8:5-17.

Kusanya muhtasari wako wa kazi ya usomaji ya wiki iliyopita, yaani, jibu lako lenye maelezo machache kuhusu mambo muhimu uliyoyaona katika vitabu ulivyoelekezwa kusoma, yaani hoja kuu ambazo waandishi walitaka kuziwasilisha (taz. Fomu ya Ripoti ya Usomaji).

Kazi za kukusanya

2

MIFANO YA REJEA

Kufanya Mungu Ajulikane

Tunapataje kufahamu mambo mbalimbali? Tunajuaje kwa uhakika kwamba kiti ni chekundu, au kwamba kuna kitu kama “wekundu”, au hata kitu kama rangi? Katika zama za sasa, hata kutazama kitu kwa macho yetu wenyewe si jambo la kutegemewa kabisa kwa sababu teknolojia inaathiri kwa kiwango kikubwa uwezo wetu wa kutambua nini ni halisi na nini si halisi. Filamu na picha zinaweza kubadilishwa bila kugundua kabisa kiasi kwamba hata wale wanaoitwa “wataalamu” wakati mwingine hawawezi kugundua kwamba zimebadilishwa. Msemo wa zamani, “kuona ni kuamini” unazidi kupoteza maana na usahihi wake. Epistemolojia ni elimu ya kitaaluma inayojaribu kufafanua maarifa ni nini na jinsi tunavyoweza kuyapata na kuyatathmini. Kuna njia nyingi za kujua mambo. Kwa mfano: • Uchunguzi na upimaji –Hii ni njia ambayo wanasayansi hutumia kufahamu mambo. • Sababu, mantiki, na tafsiri – Hii ni njia ambayo wanafalsafa hutumia kufahamu mambo. • Uzoefu, hisia, dhahania, ufahamu, na mawazo juu ya jambo fulani – Hii ni njia ambayo wasanii hutumia kufahamu mambo. Kila moja ya njia hizi za kujua ina uzuri na udhaifu fulani lakini zote hizi zina mapungufu makubwa linapokuja suala la kumjua Mungu. (Baadhi ya mapungufu

1

Made with FlippingBook Digital Proposal Maker