Mungu Roho Mtakatifu, Kitabu cha Mwanafunzi, Capstone Module 14 Swahili Student Workbook

7 2 /

M U N G U R O H O M T A K A T I F U

Hitimisho

» Roho Mtakatifu huwaleta watu kwenye ufahamu wa hitaji lao kwa Kristo kupitia huduma yake ya kuhakikisha. » Toba ni tendo la Mungu la neema kwa njia ya Roho wake, si tendo rahisi litokanalo na juhudi za kibinadamu. Hakuna mwanadamu anayelitafuta, kuliamini, kulielewa, na kulikubali Neno la Mungu pasipo huduma hai ya Roho Mtakatifu. » Toba ya kweli inahusisha kugeuka kutoka katika dhambi na kuingia katika badiliko la kusudi linaloleta badiliko la nia, moyo, na utashi. Maswali yafuatayo yaliandaliwa ili kukusaidia kupitia yaliyomo katika sehemu ya pili ya video. Ni vigumu kwa watu kukubali kwamba hali yao ya dhambi inawafanya wasiweze kumtafuta Mungu kwa kumaanisha, kuelewa kweli yake, na kukubali wokovu wake kwa hiari yao wenyewe. Viongozi wa Kikristo wanapaswa kuweka wazi ukweli kwamba ni Roho wa Mungu pekee anayeweza kumwonyesha mtu hali yake halisi na kumvuta kwa Kristo. Uhakikisho na toba havitokani na tendo la uamuzi wa kibinadamu bali hutokana na huduma ya neema ya Roho Mtakatifu. Jibu kwa uwazi na kwa ufupi iwezekanavyo, na tumia Maandiko kujenga hoja zako. 1. Tuna ushahidi gani wa kimaandiko kwamba watu hawawezi kutubu na kumtafuta Mungu mbali na kuvutwa na Roho Mtakatifu? 2. Kuhakikishwa kwa habari ya dhambi maana yake nini? Je, Roho Mtakatifu anajukumu gani katika kuwahakikisha watu kwa habari ya dhambi? 3. Neno la Kiebrania shubh linamaana gani? Neno la Kiebrania nâcham linamaana gani? Neno la Kiyunani metanoia linamaana gani? Ni kwa jinsi gani kila moja ya maneno haya linatusaidia kuelewa kwa ukamilifu zaidi maana ya kibiblia ya toba? 4. Toba inahusisha kugeuza utu wote wa mwanadamu kumwelekea Mungu. Je, toba ina maana gani kuhusiana na nia, moyo, na utashi? 5. Taja baadhi ya mambo yanayothibitisha kwamba kweli mtu ametubu. 6. Kuna tofauti gani kati ya “huzuni ya kimungu” na “huzuni ya kidunia”? 7. Kuna uhusiano gani kati ya “toba” na “matunda yatokanayo na toba”?

2

Sehemu ya 2

Maswali kwa wanafunzi na majibu

Made with FlippingBook Digital Proposal Maker