Mungu Roho Mtakatifu, Kitabu cha Mwanafunzi, Capstone Module 14 Swahili Student Workbook
/ 7 3
M U N G U R O H O M T A K A T I F U
MUUNGANIKO
Somo hili linaangazia jinsi kazi ya unabii ya Roho Mtakatifu inavyotuwezesha kuifahamu na kuitikia Kweli. Roho hutupatia kweli kuhusu Mungu katika maneno ya kibinadamu na kisha hutuwezesha kuyaelewa na kuyakubali maneno hayo. Bila huduma ya kinabii ya Roho Mtakatifu, hakuna mtu ambaye angeweza kumjua Mungu au kuelewa jinsi ya kupatanishwa naye kupitia mwanawe. ³ Ujuzi wa Mungu hauwezi kutokana na jitihada za kibinadamu, bali hutokana azimio la Mungu la kujifunua kwetu. Mungu amejifunua mwenyewe kwetu na kuyafunua makusudi yake kwetu kupitia maneno ya kinabii yaliyovuviwa na Roho wake Mtakatifu. ³ Maandiko ndiyo mamlaka kuu kwa ajili ya kutathmini madai yote kuhusu Mungu na Kweli yake. Roho Mtakatifu aliyavuvia Maandiko, akiwaongoza waandishi ili maneno waliyoandika yadhihirishe Kweli ya Mungu. Hakuna mwandishi wa Maandiko aliyevumbua mwenyewe kweli alizoziandika, bali wote walizipata kupitia ufunuo wa kinabii. Kwa mantiki hii ya msingi kabisa, Maandiko yote ni unabii. ³ Ufunuo wa kinabii huja kupitia huduma ya moja kwa moja ya Roho Mtakatifu. Nabii ni mtu ambaye Roho Mtakatifu anakaa juu yake na ufunuo wa kinabii ni karama kutoka kwa Roho. ³ Madai yoyote ya mwongozo wa kinabii leo ni lazima yapimwe na kutathminiwa kwa kuzingatia Maandiko ambayo ndiyo kipimo kilicho hakikishwa cha ukweli kwa watu wote, nyakati zote na mahali pote. ³ Roho huangazia (huweka wazi maana ya) Maandiko ambayo aliyavuvia. Roho huangazia Maandiko kupitia huduma ya kufundisha ambayo ametoa kwa Kanisa lake na kupitia kazi yake ya ndani katika akili na mioyo ya watu wanaolisikia Neno la Mungu. ³ Roho Mtakatifu ndiye njia ambayo Mungu huwavuta watu kwake. Hakuna mwanadamu anayetafuta, kuliamini, kulielewa, na kulikubali Neno la Mungu pasipo utendaji kazi wa huduma ya Roho Mtakatifu katika maisha yake. ³ Yesu alisema wazi kwamba kazi ya Roho Mtakatifu ni kuuhakikisha ulimwengu kwa habari ya dhambi. Huduma ya Roho Mtakatifu humwezesha mtu kutambua kwamba yeye ni mwenye dhambi, mwenye hatia mbele za Mungu na anastahili adhabu. Huduma ya uhakikisho ya Roho Mtakatifu inaondoa visingizio na kujihesabia haki, inazalisha hali ya kuchukia dhambi na kujuta kwa kweli kwa kutokumtii Mungu.
Muhtasari wa Dhana Kuu.
2
Made with FlippingBook Digital Proposal Maker