Mungu Roho Mtakatifu, Kitabu cha Mwanafunzi, Capstone Module 14 Swahili Student Workbook

/ 8 9

M U N G U R O H O M T A K A T I F U

3. Kuzaliwa upya kunatufanya tuwe hai, hakutufanyi tufikie ukombavu bila jitihada zozote.

a. Mfano wa kuzaliwa unatufundisha kwamba tendo la kuokoka linahitaji kufuatiwa na ukuaji thabiti kuelekea ukomavu. Kama ambavyo hatuzaliwi kimwili tukiwa tumekomaa, vivyo hivyo hatuzaliwi upya tukiwa tumekomaa (1Pet. 2:2). Ingawa tunatakaswa (tukiwa tumetengwa kwa ajili ya Mungu) pale tunapookoka, ni lazima tukue katika Kristo (Efe. 4:15, 2 Pet. 3:18).

Dokezo kwa ajili ya Huduma

Kuwatunza Wakristo wachanga ni sawa na kuwatunza watoto wachanga. Maisha mapya yanakuja kama muujiza lakini lazima yalelewe ili yaweze kuwa na afya njema na kukua.

b. Mstari wa Msingi: 1 Petro 2:2

4. Kuzaliwa upya kwa mtu mmoja mmoja ni sehemu ya kazi kubwa zaidi ya Roho Mtakatifu ya kutengeneza upya vitu vyote.

3

a. Mpango wa Mungu wa wokovu sio tu kuokoa watu kutoka kwenye kifo, bali ni kufanya upya kila kitu ambacho kimepata madhara, kupotoshwa na kuharibiwa. Mungu yuko katika mchakato wa kuiokoa sayari yetu na ulimwengu wetu na wokovu wetu ni sehemu ya mchakato huo mkubwa zaidi.

b. Mathayo 19:28 - “Amin nawaambieni, wakati wa kufanywa upya [ palingenesia = kuzaliwa upya] vitu vyote” [NEN], (ling. Matendo 3:19-21; Rum. 8:19-24).

c. Kuzaliwa upya huku kwa vitu vyote (yaani, uumbaji wote kufanywa upya) kumetabiriwa katika Agano la Kale na Agano Jipya (taz. kwa mfano, Isaya 11:6-9 na Ufunuo 21:1-5).

d. Kufanywa upya huku kwa siku zijazo kwa vitu vyote ni upanuzi wa kazi ya sasa ya Roho Mtakatifu ambaye daima anaendelea kuhifadhi na kufanya upya viumbe vyote (Zab. 104:27-30).

Made with FlippingBook Digital Proposal Maker