Mungu Roho Mtakatifu, Kitabu cha Mwanafunzi, Capstone Module 14 Swahili Student Workbook
9 0 /
M U N G U R O H O M T A K A T I F U
III. Roho Mtakatifu Anatufanya Kuwa Wana
Katika ulimwengu wa Waroma, kuasili (kufanywa mtoto wa familia fulani) kulikuwa ni “utaratibu ambao kwao mtu alihamishwa kutoka katika mamlaka ya baba yake wa asili na kuwa chini ya mamlaka ya baba yake mlezi; jambo ambalo lilihusisha uuzaji usio rasmi wa mtoto, na kujisalimisha kwake kutoka kwa baba wa asili kwenda kwa baba mlezi.” ( International Standard Bible Encyclopedia, Vol. One, uk. 54).
Warumi 9:26 Tena itakuwa mahali pale walipoambiwa, Ninyi si watu wangu, Hapo wataitwa wana wa Mungu aliye hai.
A. Kwa nini tunahitaji kufanywa wana na Mungu
1. Kufuatia dhambi ya Adamu, wanadamu wote waliingia chini ya mamlaka ya uovu (1 Yohana 3:8). Katika kifungu fulani cha Maandiko, Yesu anazungumza kwamba wale ambao hawajamkubali ni wana ibilisi (Yohana 8:44). Hii ndiyo sababu Biblia inazungumza kuhusu wokovu kama tendo la kubadili mamlaka tawala kutoka katika giza na kuingia katika nuru, au kutoka kuwa chini ya nguvu za shetani na kuwa chini ya nguvu za Mungu.
3
Hoja ya Paulo kwa habari ya wokovu wa Wamataifa imejengwa juu ya hoja ya kufanywa wana inayoonekana dhahiri katika andiko hili. Kwa kweli hawakuwa watu wa Mungu, na kwa sababu hiyo ni lazima waletwe katika uhusiano wa kindugu kwa uamuzi wa makusudi wa Mungu.
2. Kwa kuwa kwa asili sisi ni “wana wa ghadhabu” (Efe. 2:3), hatuwezi kudai nafasi ya asili katika familia ya Mungu. Badala yake, ni lazima tuletwe katika familia yake kwa njia ya kuasiliwa.
B. Kufanya wana (kuasili) ni kazi ya Roho Mtakatifu.
1. Warumi 8:14-17
2. Waefeso 2:18-19 (ling. Warumi 8:9)
Made with FlippingBook Digital Proposal Maker