Mungu Roho Mtakatifu, Mwongozo wa Mkufunzi, Capstone Module 14, Swahili Mentor Guide
/ 1 0 7
M U N G U R O H O M T A K A T I F U
(c) “Ubatizo wa Roho” unapokelewaje?
i) “Sharti pekee la kupokea ahadi ya Baba ni toba na imani” (Stanley M. Horton). Hata hivyo, Wapentekoste wanasisitiza kwamba imani wanayoieleza ni “imani tendaji, yenye utii” (William Menzies, Bible Doctrines, by Menzies and Horton, uk. 130). ii) Kutafuta kwa bidii katika maombi na kuwa na mtazamo wa kujisalimisha na kuwa tayari kubatizwa na Kristo katika Roho wake, na kuamini kwamba atafanya hivyo. Maombi haya kwa kawaida hufanywa mbele ya waamini wengine ambao huweka mikono juu ya yule anayehitaji kujazwa kwa kupatana katika maombi. (d) Je, nini husimama kama ushahidi au uthibitisho kwamba “ubatizo wa Roho” umetokea? Kunena kwa lugha ni ushahidi wa msingi. Nguvu za kiroho ni ushahidi endelevu. (e) “Ubatizo wa Roho Mtakatifu” unatimiza nini? Huongeza nguvu kwa ajili ya huduma, utume, na maisha matakatifu, ikijumuisha, uwezo mkubwa zaidi wa kutumia karama za rohoni, japo si hayo tu. (1) Kuna baadhi ya makanisa yanayochanganya maoni haya na yanajulikana kama makanisa ya Pentecostal-Holiness. Hii inajumuisha madhehebu kama Church of God in Christ [waumini milioni 5 Marekani, milioni 8 ulimwenguni], Church of God (Cleveland, TN), makanisa ya Apostolic Faith , na Kanisa la Pentecostal-Holiness. (2) Makanisa haya yanafundisha matukio matatu tofauti yahusuyo Roho Mtakatifu. (a) K wanza, wokovu ambapo Roho Mtakatifu anamuunganisha mtu na Kristo (jambo ambalo makanisa ya Reformed yanaita ubatizo katika Roho Mtakatifu). c. Ubatizo katika Roho Mtakatifu: mtazamo wa kanisa la Pentecostal Holiness
Dhumuni la awali la ubatizo ni kutoa nguvu kubwa zaidi kwa ajili ya kushuhudia (Mdo 1:8). ~ www.ag.org/top/ beliefs/baptism_hs/ baptmhs_01_distinct. cfm (tovuti ya Assemblies of God )
3
Made with FlippingBook - Share PDF online